Mkesha wa usiku wa kwanza wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, katika msikiti wa Amr Ibn El-Aas huko Cairo ya zamani. Picha: Reuters

Mwezi mtukufu wa Ramadhani unaanza Jumatatu huku Waislamu kote ulimwenguni wakiadhimisha mfungo wa kila mwaka kuanzia alfajiri hadi machweo.

Baada ya mwezi mpya kuandama Jumapili, viongozi wa kidini nchini Saudi Arabia, Kuwait, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu walitangaza kuwa Ramadhani itaanza Jumatatu.

Waislamu nchi nyingine nyingi zikiwemo Nigeria, Niger, Misri, Bahrain, Lebanon, Palestina na Iraq pamoja na Sudan pia wanaadhimisha mfungo kuanzia Jumatatu.

Hata hivyo, katika nchi za Jordan, Oman, Libya, Morocco na Iran, Ramadhani itaanza Jumanne, kwa vile mwezi mpya haukuthibitishwa huko Jumapili.

Huko Uturuki, Kurugenzi ya Masuala ya Kidini inategemea kuonekana kwa mwezi mpevu kutoka mahali popote duniani (ihtilaf-i metali) badala ya muandamo wake wa ndani ili kuamua mwanzo wa Ramadhani na likizo ya Eid al-Fitr, ambayo hufuata moja kwa moja Ramadhani.

Vita vya Gaza

Wakati wa Ramadhani, Waislamu kwa kawaida hujinyima chakula, vinywaji, sigara na ngono kuanzia alfajiri hadi machweo.

Katika kipindi chote cha mfungo wa mwezi huu, Waislamu wanasisitizwa kufanya maombi ya ziada hasa nyakati za usiku, kusoma Quran, kuwasaidia maskini na kujiepusha na maovu.

Katika ujumbe wake wa Ramadhani Jumapili jioni, Mfalme Salman wa Saudi Arabia alibainisha kuwa vita vinavyoendelea vya Israel dhidi ya Gaza vitaleta kivuli katika mwezi wa saumu na maombi.

Alitumia fursa hiyo kutoa wito wa kukomeshwa kwa "uhalifu wa kutisha" unaofanyika Gaza.

TRT Afrika