Wagombea urais wa Msumbiji, kutoka kushoto: Daniel Chapo, Venancio Mondlane, Ossufo Momade, na Lutero Simango. / Picha: TRT Afrika

Kuhesabu kura kunaendelea baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na mvutano wenye utulivu nchini Msumbiji ulianza siku ya Alhamisi, huku kiongozi wa upinzani tayari akidai ushindi wa moja kwa moja dhidi ya chama cha Frelimo kilichokuwa madarakani tangu kupatikana kwa uhuru kutoka kwa Ureno miaka 49 iliyopita.

Zaidi ya watu milioni 17 waliitwa kupiga kura siku ya Jumatano kumchagua rais mpya na wabunge katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, ambayo ina akiba kubwa ya gesi.

Ingawa matokeo yanatarajiwa tu baada ya wiki mbili, mmoja wa wagombea wakuu katika kinyang'anyiro cha kuchukua nafasi ya Rais anayemaliza muda wake Filipe Nyusi tayari alidai kuwa ameshinda.

"Leo asubuhi, tunapaswa kutangaza ushindi wetu katika ngazi ya kitaifa," Venancio Mondlane mwenye umri wa miaka 50, alisema kupitia mtandao wa Facebook.

Wapiga kura 'wanataka mabadiliko'

"Tunapaswa kuwa mitaani, tunapaswa kutangaza ushindi wetu," alisema Mondlane, ambaye ana ufuasi mkubwa miongoni mwa wapiga kura vijana. Hakutoa ushahidi wa kuwepo kwa makosa yoyoye kwenye mchakato wa uchaguzi, hata hivyo, na hakuna maandamano yaliyoripotiwa kufikia alasiri.

Huku chini ya asilimia 5 ya kura zikiwa zimehesabiwa, kituo cha uchunguzi kinachodai kuwa huru lakini kiliundwa na wafuasi wa Frelimo kilisema kuwa chama kilichokuwa madarakani kwa miaka 49 kilikuwa kinaongoza tena.

Wapiga kura wengi walisema wanataka mabadiliko katika nchi hiyo, ambayo bado inakumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 1976-1992 kati ya Frelimo na Renamo, ambacho sasa ni chama kikuu cha upinzani.

Lakini wachambuzi walisema Frelimo huenda akasalia mamlakani na kumweka mgombea wake asiyejulikana na asiye na uzoefu Daniel Chapo, 47, katika kiti cha urais.

Madai ya udanganyifu

Kulikuwa na madai mengi ya udanganyifu kwa upande wa Frelimo baada ya uchaguzi wa urais wa 2019 na kura ya manispaa ya 2023, ambayo ilisababisha mapigano na watu kadhaa kuuawa.

Hesabu za mapema na ambazo hazijathibitishwa kwenye mitandao ya kijamii pia zilidai kuonyesha mafanikio kwa Frelimo na Mondlane.

"Lakini cha muhimu si mwelekeo wa uchaguzi bali kile ambacho tume ya uchaguzi itasema," alisema mtafiti Borges Nhamirre kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Usalama yenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini.

Mondlane, ambaye alijiondoa kutoka kwa chama cha Renamo mwezi Juni na anaungwa mkono na chama kidogo cha Podemos, angehitaji kuthibitisha uldanfganyifu katika upigaji kura kama angetaka wafuasi wajiunge na mwito wake wa maandamano, alisema.

Hakuna matukio makubwa

Mgombea huyo hata hivyo anaweza kuipita chama cha Renamo kama chama kikuu cha upinzani, hata kama Frelimo hatokubali kuruhusu duru ya pili ya upigaji kura, Nhamirre aliongeza.

Ingawa hakuna matukio makubwa yaliyoripotiwa siku ya kupiga kura, waangalizi wa uchaguzi walibaini kasoro kadhaa ikiwa ni pamoja na wapiga kura kuonekana wakiwa na karatasi mbili za kupigia kura na waangalizi wa upinzani kuzuiwa kuingia katika baadhi ya vituo vya kupigia kura.

"Sasa ni kwamba udanganyifu utaanza, kwa njia ya kutangaza matukio," mchambuzi mmoja ambaye hakutaka kutajwa kutotajwa jina."

Ikiwa Venancio ataonyesha uongozi thabiti, hali itakuwa ya wasiwasi haraka sana," alisema, akizungumzia "ukimya mwingi na woga kutoka upande wa serikali."

Rais ahimiza utulivu

Mnamo 2019, Frelimo anayetumia mfumo wa Marxist alichukua asilimia 73% ya kura.

Wataalamu wamesema tume ya uchaguzi inaweza kutangaza matokeo ya kawaida zaidi wakati huu ili kuepusha vurugu lakini kuiweka Frelimo mamlakani, ambayo imekuwa ikishikilia tangu uhuru kutoka kwa Ureno mnamo 1975.

Nyusi ambaye amefikia mwisho wa kikomo cha mihula miwili, Jumatano alitoa wito kwa pande zote kuwa watulivu na kuepuka kudai kujua matokeo kabla ya kutangazwa.

Changamoto kubwa kwa serikali yoyote ijayo ni uchumi wa taifa hilo la Bahari ya Hindi, linalolemewa na umaskini na vimbunga vya mara kwa mara na ukame.

Ilikuwa na matumaini ya kuimarika kiuchumi baada ya akiba za gesi kugunduliwa kaskazini mwaka wa 2010 lakini uasi wa wanamgambo katika eneo hilo umezuia maendeleo ya miradi ya uchimbaji.

TRT Afrika