Wanaume 17, raia wa China wamekamatwa kwa tuhuma za kuendesha mgodi haramu wa dhahabu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mamlaka ilisema hapo Ijumaa, wakati serikali ikiendelea na msako mkali wa uchimbaji wa madini yake bila leseni.
Wanaume hao waliletwa katika mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa kutangaza kuzuiliwa kwao Bukavu, mji mkuu katika jimbo la Kivu Kusini linalokumbwa na mapigano. Walikaa kwenye viti bila vizuizi na hawakuzungumza na waandishi wa habari.
Watu hao walikamatwa baada ya ujumbe wa serikali kufanya ziara bila kutangazwa kwenye eneo la mgodi katika kijiji cha Karhembo siku ya Alhamisi, waziri wa fedha wa jimbo hilo na kaimu waziri wa madini, Bernard Muhindo, alisema.
“Tuliomba watuwasilishe hati za kampuni hapakuwa na hati, sifuri, hakuna cheti, hadhi, kitambulisho cha taifa, hakuna,” Muhindo alisema.
Takriban raia 60 wa China walikuwa kwenye eneo hilo na maafisa waliwashikilia 17 ambao walionekana kuwa wasimamizi, pamoja na baadhi ya watu kutoka Congo na nchi jirani ya Burundi, aliongeza.
Ubalozi wa China mjini Kinshasa haukujibu mara moja ombi la Reuters la kutoa maoni. Ubalozi wa Burundi umesema bado unasubiri maelezo kutoka kwa mwakilishi wake mjini Bukavu.
Nchi hiyo ya Afrika ya kati inasema imekuwa ikijitahidi kuzuia makampuni yasiyo na leseni na katika baadhi ya makundi yenye silaha kunyonya akiba yake tajiri ya cobalt, cooper, dhahabu na madini mengine.
Ushindani kuhusu shughuli za uchimbaji madini umechochea mapigano katika eneo hilo linalopakana na Rwanda.