Wanamgambo wa kikundi cha M23 wameendelea kushika hatamu katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku miji mingi zaidi ikiangukia mikononi mwa waasi hao, chanzo kimoja kimeliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumapili.
Kinshasa inaituhumu Rwanda kwa kukiunga mkono kikundi cha Kitutsi cha M23 ambacho kinashikilia maeneo mengi ya mashariki ya DRC, tuhuma zilizopingwa na Kigali.
Siku ya Jumapili, kikundi cha M23 kiliingia kwenye mji wa Kirumba, kaskazini mwa Kivu, eneo lililotawaliwa na vurugu toka mwaka 2021.
Kirumba ni mji mkubwa kusini mwa eneo la kibiashara la Lubero lenye wakazi zaidi ya 120,000.
Kuelekea kaskazini
"Tunasikitika kuona kuwa toka jana, sehemu kubwa ya mji uko mikononi mwa M23," alisema ofisa mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumapili.
Kulingana na ofisa huyo, kikundi hicho kilikuwa kinaelekea kaskazini mwa mji huo.
Siku ya Jumamosi, kikundi cha M23 kilishikilia mji wa kimkakati wa Kanyabayonga, huku maeneo mengine yakiwa chini ya udhibiti ya waasi hao.
Kanyabayonga ni eneo lenye wakazi zaidi ya 60,000 huku wengine wengi wakiwa wamekimbia eneo hilo kutokana na uwepo wa waasi hao.
Rais aitisha kikao cha dharura
Mji huo unachukuliwa kuwa njia ya kuelekea Butembo na Beni kaskazini, ngome za kabila la Nande na vituo vikuu vya kibiashara.
Ipo katika eneo la Lubero, mji wa nne kaskazini mwa Kivu ambalo waasi hao walitumia kuingilia baada ya Rutshuru, Nyiragongo na Masisi
Siku ya Jumamosi, Rais Felix Tshisekedi aliitisha baraza la ulinzi la taifa.
Wakati wa hotuba ya kuadhimisha siku ya uhuru wa nchi hiyo, Tshisekedi alisema "maelekezo ya wazi na madhubuti yametolewa kwa ajili ya kulinda uadilifu wa eneo la nchi yetu", pasipo kutoa maelezo zaidi.
Uhamisho mkubwa
Miji mingine karibu na Kanyabayonga pia yapo chini ya udhibiti wa M23, kulingana na vyanzo vya kiusalama.
Eneo la DRC lenye utajiri wa madini limeshuhudia vurugu za miaka 30 kutoka vikundi vyenye silaha.
Katika ripoti yake ya kila mwezi siku ya Ijumaa, ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, eneo hilo limeshuhudia uhamaji mkubwa wa watu.