Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Sudan Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan amefanya mkutano na Rais wa Sudan Salva Kiir, mjini Juba kujadiliana kuhusu mgogoro wa Sudan.
Mapigano yalizuka mjini Khartoum mwezi Aprili kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya RSF na mzozo kulipuka tangu wakati huo na kugeuka kuwa mapigano ya wazi katika mji mkuu wa Khartoum na maeneo mengine.
"Sisi Sudan tunaona kuwa Sudan Kusini ndiyo nchi bora ya kutafakari mgogoro wa Sudan, kwa sababu tumekuwa nchi moja kwa muda mrefu na tunajuana, tunajua matatizo na tunajua mahitaji yetu", Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Ali al-Sadiq alisema.
Kwa upande wake, Waziri wa masuala ya baraza la mawaziri wa Sudan Kusini Dkt. Martin Elia Lomuro alisema ni kwa manufaa ya Sudan Kusini kutafuta suluhu la mgogoro wa Sudan.
"Inafahamika wazi kuwa Rais Kiir ndiye kiongozi pekee ambaye ana uzoefu juu ya Sudan na anaweza kutafuta suluhu la mgogoro wa Sudan". Dkt. Lomuro alisema.
Mapigano nchini Sudan yaliyoanza Aprili 15 yamesababisha mmiminiko wa watu waliokimbia nchi hiyo kuelekea nchi jirani, ikiwemo Sudan Kusini.
Zaidi ya watu milioni 4 wamesalia kuwa wakimbizi nchini Sudan, milioni 2.5 wa ndani na milioni 2.2 katika nchi jirani, kulingana na UN.