Somalia imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa usalama kwa miaka mingi / Picha: Reuters

MOGADISHU, Somalia.

Takriban magaidi 44 wa al-Shabaab waliuawa katika operesheni ya usalama katika eneo la Lower Shabelle nchini Somalia, Wizara ya Habari ya nchi hiyo ilisema Jumamosi.

Operesheni hiyo iliendeshwa siku ya Ijumaa na wakala wa kitaifa wa kijasusi na usalama unaoungwa mkono na washirika wa kimataifa wa Somalia kwenye viunga vya Kurtowarey, mji mdogo ulioko kilomita 208 (maili 229) kusini magharibi mwa mji mkuu wa taifa hilo Mogadishu.

Kulingana na Naibu Waziri wa Habari wa Somalia Abdirahman Yusuf Adala, makamanda wakuu wa al-Shabaab walikuwa miongoni mwa magaidi waliouawa katika operesheni hiyo.

Vikosi vya usalama vya Somalia vimekuwa vikiendesha operesheni dhidi ya al-Shabaab tangu Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud kutangaza "vita vya kila namna" dhidi ya kundi hilo la kigaidi mwaka jana.

Kundi hilo limekuwa likipigana dhidi ya serikali ya Somalia na ujumbe wa Umoja wa Afrika tangu mwaka 2007.

Somalia imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa usalama kwa miaka mingi, huku vikundi vya kigaidi vya al-Shabaab na Daesh/ISIS vikiwa vitisho vikuu.

TRT Afrika