Nairobi, Kenya
Idadi ya vifo vinavyotokana na mafuriko yanayosababishwa na El Nino nchini Kenya, imeongezeka hadi kufikia 136 baada ya watu 16 zaidi kufa kati ya Jumatano na Alhamisi, mamlaka ilisema.
Aidha, ikithibitisha vifo hivyo vya hivi karibuni, Wizara ya Mambo ya Ndani, pia imesema kuwa zaidi ya nyumba 92,400 na watu 462,100 wameathiriwa na mafuriko.
Raymond Omollo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Kenya, alisema kuwa serikali inafanya kazi ya kupeleka chakula kwa watu walizoathiriwa.
"Kwa bahati mbaya, katika saa 24 zilizopita, vifo 16 vimeripotiwa, na kuongeza idadi ya watu waliofariki hadi 136," Omollo alisema.
"Usambazaji wa chakula unaendelea katika kaunti zilizoathirika," alimaliza.
Mbali na vifo vya watu wengi, mafuriko hayo pia yameangamiza mifugo, na takriban wanyama 2,500 wamekufa ndani ya kipindi cha muda mfupi.
Mbali na changamoto ya mafuriko, mvua hizo pia zimesababisha maporomoko ya ardhi na udongo nchini Kenya.
Nchi kama Somalia na Ethiopia nazo pia zimeshuhudia madhara kama hayo ikiwemo uharibifu wa miundombinu.