Victoria Falls ni mtiririko yenye mandhari ya kuvutia na fahari yenye kustaajabisha kwenye Mto Zambezi / Photo: AP

Victoria Falls-iliyopo katika mto Zambezi, ambao ndio mpaka wa Zimbabwe na Zambia ina maporomoko makubwa zaidi ya maji duniani.

Ni mtiririko yenye mandhari ya kuvutia na fahari yenye kustaajabisha kwenye Mto Zambezi.

Kabila la Kololo linaloishi katika eneo hilo linaitwa 'Mosi-oa-Tunya' ikimaanisha 'Moshi Utoao Ngurumo' kutokana na maji hayo yanayoporomoka kwa kasi huku yakitoa kelele za ajabu.

Sauti ya maji haya inaweza kusikika umbali wa zaidi ya kilomita 40.

Victoria Falls ina upana wa mita 1708 na lita milioni 500 zinaporomoka kwa dakika katika kina cha urefu wa mita 61.

Victoria Falls baada ya kuporomoka, maji yake yanaweza kuruka kwa zaidi ya urefu wa mita 400/ Picha: Reuters 

Mtiriko huu wa maji unashuhudiwa Zimbabwe upande wa magharibi na Zambia upande wa mashariki, na unaweza kufikiwa kwa urahisi kutoka nchi zote mbili kupitia Mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe au Livingstone nchini Zambia.

Victoria Falls baada ya kuporomoka, maji yake yanaweza kuruka kwa zaidi ya urefu wa mita 400.

Ukungu wa maji haya huhifadhi mfumo wa ikolojia unaofanana na msitu wa mvua ulio karibu na maporomoko.

Maporomoko haya ya karne kadhaa pia yamesababisha mmomonyoko wa udongo, madimbwi kadhaa ya miamba mojawapo likiwa ukingoni! Kimepewa jina la ' devil's pool'.

Dimbwi hilo liko karibu na Kisiwa maarufu cha Livingstone kilicho kwenye ukingo wa Maporomoko ya Victoria.

Hapa inataka ujasiri wa kupiga mbizi katika maji haya. Wageni wanaruhusiwa kutembelea eneo la dimbwi kati ya Agosti na katikati ya Januari tu kwani wakati huo maji yanakuwa katika kina cha chini ambacho ni salama.

Maporomoko ya Victoria yanazidi kukumbwa na changamoto ya ukavu na joto zaidi. Wakati eneo bado linapata takriban mvua zilezile kila mwaka, wataalamu wanasema mvua hizo hunyesha kwa muda mfupi.

Viwango vya joto, pia, vinaongezeka na kutishia mali hii ya asili ambayo ni kivutia kikubwa cha utalii kwa Zimbabwe na Zambia.

TRT Afrika