Uturuki yamkamata kiongozi wa Ujerumani wa kundi la kigaidi la PKK

Uturuki yamkamata kiongozi wa Ujerumani wa kundi la kigaidi la PKK

Saim Cakmak amehusika na shughuli za kikundi hicho nje ya nchi.
Cakmak amekamatwa Istanbul katika operesheni iliyoendeshwa na intelijensia ya Uturuki./ Picha: AA  

Saim Cakmak, moja wa viongozi wa kikundi cha kigaidi cha PKK nchini Ujerumani, amekamatwa Istanbul katika operesheni iliyoendeshwa na vyombo vya ulinzi na intelijensia ya Uturuki.

Cakmak, aliyedhamiria kuhusika katika shughuli za shirika nje ya nchi, baadaye alifikishwa kortini na kukamatwa rasmi, vyanzo vya usalama vilisema Jumatano.

Vikosi vya usalama vya Uturuki vimewakata makali magaid sita wa PKK katika operesheni ya anga katika eneo la Hakurk, kaskazini mwa Iraq, Wizara ya Ulinzi ya imesema siku ya Jumatano.

"Vikosi vya usalama vya Uturuki vimeendelea kuwateketeza magaidi wa kaskazini mwa Iraq," imesema. "Vita vyetu dhidi ya ugaidi vitaendelea kwa ufanisi."

Magaidi wa PKK mara nyingi hujificha kaskazini mwa Iraq ili kupanga mashambulizi ya kuvuka mpaka huko Uturuki.

Katika kampeni yake ya takriban miaka 40 ya ugaidi dhidi ya Uturuki, PKK - iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, na Umoja wa Ulaya, imehusika na vifo vya zaidi ya watu 40,000, wakiwemo wanawake na watoto, hususani wachanga.

YPG ni zao la PKK la Syria.

TRT Afrika