Kiua vijasumu ni dawa zinazotumiwa kuzuia na kutibu maambukizi ya bakteria.
Shirika la afya duniani, WHO, linaonya kuwa ni muhimu kubadili jinsi inavyoagizwa na kutumika ili dawa hizi ziwe na matokeo yanayotarajiwa, kwani kumekuwa na visa vya dawa hizi kutofanya kazi na kutoa tiba inayohitajika.
Ukinzani wa viua vijasumu hutokea wakati bakteria wanapobadilika kutokana na matumizi ya dawa hizi.
Bakteria hawa wana uwezo wa kutosha kutafuta njia ya kuepuka athari ya dawa kwa sababu wanataka kuishi.
Je, WHO inatoa ushauri gani kwa matumizi ya dawa hizi za viua vijasumu?
- Jaribu kutumia kiuavijasumu tu kama ilivyoagizwa na daktari wako au mtoa huduma wako wa afya
- Kamilisha kipimo cha kiuavijasumu kulingana na maagizo yaliyotolewa na daktari
- Hakikisha kuwa haushiriki dawa yako ya viuavijasumu na familia au marafiki kwa sababu inahitaji kutolewa kwa kuzingatia mwongozo, kulingana na ishara na dalili mahususi ambazo kila mtu anazo
- Maambukizi fulani ya virusi, kwa kweli hayahitaji mautmizi ya dawa hiyo
- Kumbuka kwamba tuna bakteria wanaoishi kwenye ngozi yetu, wanaishi katika mfumo wetu wa utumbo
- Kwa hivyo kuwaangazia bakteria hawa kwa vipimo visivyofaa au dozi zisizo kamili za viuavijasumu huchokoza bakteria kwa njia fulani tu, inahuiruhusu kuunda mbinu za kutotibiwa na viuavijasumu hivi. Kwa hivyo hatari ni kwamba tutaanza kuunda bakteria wenye nguvu zaidi.
TRT Afrika