Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) / Picha: AP

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) hadi tarehe 30 Aprili 2024.

Azimio nambari 2726, lililoungwa mkono kwa kauli moja na baraza la wanachama 15, liliamua kuongeza muda wa UNMISS na kuidhinisha ujumbe huo kutumia njia zote muhimu kutekeleza majukumu yake.

Baraza hilo, lilipitisha azimio la kuidhinisha "mabadiliko ya kiufundi" kwa mamlaka ya UNMISS. Azimio hilo, Baraza lilisema, lilipitishwa chini ya Sura ya VII ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Marekebisho ya kiufundi, kulingana na Baraza la Usalama, yataruhusu muda zaidi kwa wajumbe wa baraza kutathmini utayari wa uchaguzi wa Sudan Kusini na kujadili upanuzi mkubwa wa mamlaka ya ujumbe huo, ambao unajumuisha usaidizi wa kiufundi kwa uchaguzi wa Sudan Kusini.

Sudan Kusini inapanga kufanya uchaguzi Disemba 2024.

Baraza la UN liliidhinisha UNMISS kutumia njia zote zinazohitajika kutekeleza majukumu yake.

UNMISS kwa sasa inatoa usaidizi wa kiufundi, ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo, na usaidizi wa vifaa kwa ajili ya mchakato wa uchaguzi na usaidizi wa usalama ili kuwezesha mzunguko wa uchaguzi, miongoni mwa mengine.

TRT Afrika