Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa litafanya kikao cha dharura katika siku zijazo kujadili matukio ya hivi karibuni ya kuchomwa moto kwa kitabu kitakatifu cha Quran barani Ulaya, msemaji wa baraza hilo alisema Jumanne.
"Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa litafanya mjadala wa dharura kujadili ongezeko la chuki za kidini vilivyopangwa kimakusudi na hadharani, kama inavyodhihirishwa na kudhalilishwa kwa Quran tukufu katika baadhi ya nchi za Ulaya na nyinginezo," msemaji wa baraza hilo Pascal Sim aliwaambia waandishi wa habari.
Pascal Sim alitoa ombi kwa ajili ya mkutano huo kutoka Pakistan kwa niaba ya baadhi ya wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu.
"Mjadala wa dharura utaitishwa wiki hii kwa tarehe na wakati utakaoamuliwa na ofisi ya Baraza la Haki za Kibinadamu linalokutana leo," alisema.
Tukio la Uswidi
Haya yanajiri baada ya kuchomwa kwa nakala ya Quran nchini Uswidi siku ya Jumatano, na kusababisha msukosuko wa kidiplomasia katika ulimwengu wa Kiislamu.
Salwan Momika, mwenye umri wa miaka 37, alikanyaga kitabu kitakatifu cha Waislamu na kuwasha moto kurasa kadhaa wakati Waislamu kote ulimwenguni walianza kuadhimisha sikukuu ya Eid al-Adha.
Hii ilifanyika huku ibada ya kila mwaka ya hija ya kwenda Mecca nchini Saudi Arabia ikielekea ukingoni.
Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa lenye makao yake makuu mjini Geneva, ambalo linakutana katika kikao hadi Julai 14, litabadilisha ajenda yake ili kuandaa mjadala wa dharura, shirika la habari la AFP linaripoti.
Kuna wajumbe 47 wa Baraza la Haki za Kibinadamu.
Chombo hicho cha juu cha haki za Umoja wa Mataifa kwa sasa kiko katika kikao chake cha pili cha kawaida kwa mwaka.