Ulimwengu haupaswi kupuuza janga kubwa la kibinadamu linaloikumba Sudan

Ulimwengu haupaswi kupuuza janga kubwa la kibinadamu linaloikumba Sudan

Bila maslahi ya kimataifa na shinikizo la umma, hali nchini Sudan bila shaka itazidi kuwa mbaya
Zaidi ya nusu milioni ya waliokimbia makazi yao wamekimbilia nchi jirani / NRC / Ahmed Omer

Sudan iko katika mwezi wa tatu wa migogoro na mateso yasiyoisha. Hali ya karibu watu milioni tatu waliokimbia makazi yao inazidi kuwa mbaya.

Zaidi ya nusu milioni ya waliokimbia makazi yao wamekimbilia nchi jirani. Wanakimbia kutokana na vurugu zinazoongezeka, mara nyingi hubeba mali zao kwenye mfuko mmoja wa plastiki, kwa wale waliobahatika kufanya hivyo nimeona hofu yao.

Wajane na watoto wakiwa wamejaa majeraha ya risasi katika miili yao, na watu wengi wasiohesabika waliondoka bila chochote.

Wakimbizi kutoka Nchini Sudan Kusini, Eritrea, Ethiopia, na Syria pia ni sehemu ya msafara huu, wote wakitafuta usalama, lakini wakikumbana na maovu ya kila siku ya milipuko ya mabomu na mauaji inayoendelea kuwaandama.

Wajane na watoto wakiwa wamejaa majeraha ya risasi katika miili yao, na watu wengi wasiohesabika waliondoka bila chochote. Picha : NRC

Simulizi hii ya kuhuzunisha inaendelea kusahaulika katika mazungumzo ya kimataifa, bila kuzingatia uwezekano wowote wa kupatikana suluhisho na kuhujumu uwezekano wa kupatikana amani katika siku za hivi karibuni.

Hivi majuzi, vyombo vya habari vya kimataifa vimeangazia mgahawa ulioathiriwa na mashambulizi ya anga nchini Ukraine au Duka la simu la Apple lililoporwa nchini Ufaransa.

Wakati masoko makubwa ya Khartoum ambayo ni moyo wa Uchumi katika moja ya nchi kubwa zaidi barani Afrika, yameharibiwa na kuachwa vifusi na majivu kutokana na ghasia zinazoendelea nchini humo ambapo kwa namna moja au nyingine hayazingatiwi.

Nyumba, hospitali, na maghala yaliyojaa misaada muhimu ya kibinadamu yameporwa na kuharibiwa vibaya kote Khartoum, Kordofan Kaskazini na Darfur.

Familia zinazokimbia kutoka Darfur ni nyingi na nyingine zimekuwa zikilengwa na kukumbana na kupigwa risasi walipokuwa wakijaribu kutorokea Chad kwa miguu.

Kupuuza huzaa matokeo mabaya. Mkutano wa hivi karibuni wa misaada kwa Sudan ulipungua nguvu kwa kiasi kikubwa, na kuongeza nusu tu ya fedha zinazohitajika kushughulikia janga hili la kibinadamu.

Wakimbizi wanaokimbia kutoka pande zote za Sudan wanapokea msaada mdogo au hawapati kabisa msaada kutokana na rasilimali chache na vikwazo vinavyoongezeka vya ukiritimba vinavyozuia utoaji wa misaada na harakati.

Mapigano yamezidi kusambaa, huduma muhimu zinaporomoka, msimu wa mvua huleta mafuriko na magonjwa, hali ya njaa inazidi kuwa kubwa, na hali inazidi kuachwa nje ya jarida au ajenda ya kidiplomasia.

Huenda vyombo vya habari na jumuiya ya kimataifa wanatafuta hadithi ya kusisimua, zenye mwanga wa matumaini ya kuunga mkono, ili kuendelea kuangazia hadithi hiyo?

Kusafiri kote nchini kumekuwa kwa tabu, naona kila siku ushujaa na uthabiti wa mashujaa wa ndani wa Sudan. Ikiwa ulimwengu unatafuta cheche za matumaini, zisitazame mbali zaidi ya mashujaa wa ndani wa Sudan.

Vijana hawa jasiri wa kujitolea wameinuka kukabiliana na changamoto, wakijumuisha nguvu za jumuiya zao katikati ya machafuko.

Vitendo vyao vya kutia moyo vinalazimisha mashirika ya misaada, sio tu kuwaunga mkono bali pia kutimiza mipango yao ya kukidhi mahitaji yanayoongezeka.

Nia kamili na roho ya kizazi kipya inapaswa kuwa mwanga unaosaidia kuiongoza Sudan kutoka kwenye giza hili – katika unafuu wa haraka, na zaidi.

Zaidi ya watu milioni mbili wameachwa bila makao tangu vita vya Sudan kuanza mwezi Aprili Picha : NRC

Hekima ya wazee inatuambia tu kwamba tunahitaji kuepuka zamani, kwa gharama yoyote. Hivi sasa, mwitikio wa misaada unarudi nyuma lakini unahitaji mteremko kwenda mbele.

Juhudi hizi za usaidizi zinazoongozwa na vijana nchini Sudan zinaweza kuimarishwa, kukuzwa na kuangazwa kwa usaidizi mpana na mshikamano.

Bila maslahi ya kimataifa na shinikizo la umma, hali itakuwa mbaya zaidi. Uthabiti wa eneo hilo unazidi kudorora, huku kukiwa na mwangwi wa ukatili mkubwa kutoka katika siku za nyuma za Darfur.

Kila juhudi za misaada inayoongozwa na raia wa Sudan lazima iimarishwe, vikwazo vyote kwa misaada ya kibinadamu viondolewe, na viongozi wa dunia lazima wajipange kukomesha umwagaji damu unaoendelea nchini Sudan.

Kwa hivyo wakati utangazaji wa habari wa Sudan unaweza kuwa umefikia kilele, taarifa bado haijaisha. Kwa kweli, inaweza hali kuwa mbaya zaidi kwa kuongezeka kwa mgogoro wa kibinadamu.

Juhudi za kumaliza vita vya kuidhibiti Sudan bado hazijazaa matokeo yanayotarajiwa kuashiria uwezekano wa kuendelea kuhama makwao ndani ya nchi hiyo na kuvuka mipaka yake.

Ulimwengu lazima uzingatie Sudan sasa zaidi kuliko hapo awali, na kuunga mkono wale ambao wanaweza kupanga njia mpya ya kusonga mbele.

Mwandishi ni Will Carter, ambaye ni Mkurugenzi wa Nchi wa Baraza la Wakimbizi la Norway nchini Sudan.

Kanusho: Maoni yaliyotolewa na mwandishi si lazima yaakisi maoni na sera za uhariri za TRT Afrika.

TRT Afrika