Mshambuliaji huyo wa Brazil Vinicius Junior akitokwa na machozi katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mchezo kati ya Brazil na Hispania, Machi 25, 2024 (AFP/Pierre-Philippe Marcou).  

Hivi karibuni, nyota wa soka wa Brazil Vinícius Junior aliangua kilio mbele ya waandishi wa habari kabla ya mechi na Real Madrid, akisema anahisi "kuvunjwa moyo " kuendeela kucheza mchezo huo huku maneno na nyimbo za kibaguzi zikielekezwa kwake.

Mchezaji huyo mwenye miaka 23 amezitaka taasisi zinazosimamia mchezo huo unaopendwa zaidi duniani kufanya jitihada zaidi kukomesha vitendo hivyo ndani na nje ya uwanja. Tatizo linakwenda zaidi ya soka na moja kwa moja kwenye tatizo la ubaguzi wa rangi lililojikita ndani ya Uhispania kwenyewe.

Mwaka jana, Vinicius alichukizwa na kitendo cha mashabiki wa klabu ya Valencia kutokana na ishara za nyani walizomuonesha, simu kutoka mashirika ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Hispania zilitawala milio. Mimi nilikuwa miongoni mwa watu waliopiga simu, nikijibu maswali ya vyombo vya habari bila kukoma.

Nakumbuka vizuri tu namna kila swali lilitaka kujua kama kulikuwa na ubaguzi wa rangi nchini Hispania. Jibu langu lilibakia kuwa: ndio.

Uhispania ni nchi iliyotawaliwa na ubaguzi wa rangi hasa wa kimuundo huko, kama vile ubaguzi wa kijinsia au utabaka. Mara nyingi huwa imekita mizizi katika kila eneo la jamii yetu.

Kama mtu mweusi niliyezaliwa Uhispania, nalifahamu hili kutokana na uzoefu wangu toka nikiwa mtoto mdogo, hasa wakati nikiwasaidia ndugu zangu na michakato ya uhamiaji, kunyanyaswa kwenye vizuizi vya polisi na maombi yangu ya kazi pamoja na vitisho vya kibaguzi mitandaoni.

Maisha yangu ni sheria kwa watu Weusi. Kwa miaka mingi nimekuwa nikiichambua kutoka kwa mitazamo mingi.

Nchini Uhispania, kuna taarifa chache sana kuhusu athari za ubaguzi wa rangi, lakini tunajua kwamba asilimia 80 ya makampuni ya mali ihayakubali kuwakodisha wahamiaji; huku ubaguzi wa shule ukionekana zaidi kila siku.

Pamoja na ushahidi huo, Uhispania bado inakanusha kuwepo kwa ubaguzi wa na kutuaminisha kuwa hilo ni tukio la nadra sana. Hivi majuzi, nyota wa kandanda wa nchi hiyo Carvajal, na Donato wa Brazil walisema Uhispania sio nchi ya kibaguzi. Lakini swali langu ni: je; ikiwa kweli hakuna ubaguzi nchini Uhispania, kwanini basi kumekuwepo na matukio mengi ya ubaguzi wa rangi kwa miongo kadhaa?

Linapokuja suala la soka, viongozi wanapaswa kujua zaidi. Vinicius sio mfano wa kwanza wala wa mwisho. Siku chache zilizopita, kulikuwa na mifano mitatu ya matusi ya kibaguzi: kwa Cheikh Sarr, kipa wa Rayo Majadahonda, kwa kocha wa Roma wa Sevilla, Quique Sanchez Flores, na kwa mwanasoka wa Argentina katika timu hiyo hiyo, Marcos Acuña.

Miaka 10 iliyopita, Dani Alves alitupiwa ndizi kutoka kwenye jukwaa la mashabiki. Mwaka 2006, nyota wa zamani wa Cameroon Samuel Eto'o alitaka kutoka nje ya uwanja kufuatia milio ya nyani iliyoelekezwa kwake. Zaidi ya hapo, mwaka 1993, mlinda mlango wa Nigeria Wilfred Agbonavbare alisema alisikia katika uwanja wa Real Madrid wakipiga kelele kuhusu "Ku Klux Klan" na mialiko ya kuchuma pamba.

Mwaka jana, Iñaki Williams, mchezaji wa Athletic Club de Bilbao aliyezaliwa na wazazi wa Ghana, kwa mara ya kwanza, alipeleka suala la ubaguzi wa rangi mahakamani.

Mshambuliaji wa Athletic Bilbao's Inaki Williams, kushoto, akichuana na mchezaji wa Valencia Mouctar Diakhaby katika mchezo wa Kombe la Mfalme uliofanyika mjini Bilbao, nchini Uhispania. (AP/Alvaro Barrientos).

Kawaida, wakati wa michezo huwa na kamera nyingi mashabiki waliojazana kwenye majukwaa. Wale wenye kutoka kauli za kibaguzi inafaa kuwa rahisi kuwatambua. Lakini itakuwa ni kosa kufikiri kwamba hii hutokea tu katika ngazi ya wasomi.

Matendo ya kibaguzi pia huhusisha mashabiki kwa mashabiki. Mwezi Februari, kabla ya mchezo kati ya Real Madrid na Atlético de Madrid, mtu mzima mmoja alimwambia binti wa miaka minane aliyevalia jezi ya Vinicius nje kidogo ya uwanja maneno ya kibaguzi. Miezi michache baadaye, alikamatwa.

Ninakumbuka wakati wangu nikiwa mchezaji mahiri katika Huesca, mji mdogo kaskazini mwa Uhispania, nikiwa na miaka 12 tayari nilikuwa nikisikia matusi ya kibaguzi kutoka kwa wapinzani. Na mbaya zaidi, kutoka kwa jamaa zao wazima. Miaka 20 baadaye, bado kumbukumbi hizo ziko kichwani mwangu. Maisha yangu sio ubaguzi, ni sheria kwa watu Weusi ambao wamecheza soka nchini Uhispania.

La liga inafanya nini katika yote haya? Nadhani wamekuwa wakichukua njia za mkato zisizo na athari yoyote ile. Ligi ya Uhispania imechagua kupeleka malalamiko kwa mahakama za kawaida, kuchelewesha taratibu na uwezekano wa vikwazo.

Itifaki hazizingatii athari za mashindano, kama vile kufunga majukwa, kupokonywa alama muhimu kuzima stendi na viwanja au kuchukua pointi, namna Ligi Kuu inavyofikiria kufanya.

Lakini suala kuu liko kwenye jamii yenyewe. Tunajifunza ubaguzi wa rangi kutoka kwa umri mdogo kupitia lugha, vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, na siasa au taasisi zinazoendeleza ubaguzi wa rangi. Ilimradi tusichukue nafasi ya elimu hii na maarifa ya kupinga ubaguzi wa rangi, tabia hizi zitaendelea kuwepo ndani na nje ya viwanja vya soka.

Machozi ya Vinicius katika mkutano wa waandishi wa habari yanaashiria kushindwa kwa jamii kukabiliana na tatizo la ubaguzi wa rangi.

Ni machozi ya wale ambao, kama mchezaji wa Brazil, wanaona jinsi miaka inavyosonga na maendeleo kuelekea jamii inayopinga ubaguzi wa rangi ni polepole kuliko vile tungependa. Uzoefu wake uwanjani unaonyesha shida kubwa na iliyoenea kuliko tunavyofikiria.

Hali hii inawafanya idadi ya watu wa Uhispania kuzungumza, kufikiria, kusoma na kusikiliza mabishano kuhusu rangi za watu, lazima kuwepo na majadiliano iwapo tunataka kuleta mabadiliko.

Lakini machozi ya Vinicius pia yameangazia madhara ya ubaguzi wa rangi kwa afya ya akili. Matendo yake nje ya uwanja yanaongeza wigo wa mazungumzo ya dharura na muhimu kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa huu

Hali hii inawafanya idadi ya watu wa Uhispania kuzungumza, kufikiria, kusoma na kusikiliza mabishano kuhusu rangi za watu, lazima kuwepo na majadiliano iwapo tunataka kuleta mabadiliko.

Ndoto yangu ni kwamba katika siku zijazo, mahojiano kuhusu kesi kama Vinicius' hayataanza kwa kuniuliza ikiwa Uhispania ni nchi ya ubaguzi wa rangi au la.

Ndoto yangu ni kuanza kuzungumzia kile ambacho Uhispania inafanya kuwa nchi inayopinga ubaguzi wa rangi. Hayo ndiyo mazungumzo ya kweli tunayopaswa kuwa nayo.

Moha Gerehou, ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kupitia machapisho, redio na televisheni. Yeye pia ni mwanachama wa Conciencia Afro, rais wa zamani wa SOS Racismo nchini Uhispania na mwandishi wa kitabu "Qué hace un negro como tú en un sitio como este" (Mtu Mweusi kama wewe anafanya nini mahali kama hapa?)

TRT Afrika