Kongamano hilo litafanyika mjini Johannesburg, litakuwa ni la kihistoria ambalo linalenga kuongeza hitaji la dharura la kushughulikia vitendo vya mauaji ya kiimbari vinavyoendelea vya Israel dhidi ya Wapalestina - hasa huko Gaza.
Mkutano huo ulioandaliwa na Kamati ya Uongozi ya Kupambana na Ubaguzi wa Rangi wa Afrika Kusini (SAAASC), utafanyika kuanzia tarehe 10-12 Mei na unaonyesha nia ya pamoja ya kuhamasisha hatua za kimataifa, kwa lengo la kuiwajibisha Israeli kwa uhalifu wake dhidi ya watu wa Palestina.
Kadhalika mkutano huo utaweka msingi wa kuimarisha uhamasishaji, mpangilio na uratibu wa kimataifa dhidi ya ubaguzi wa rangi na ukabila wa Israel na "kuandaa mikakati ya kina ya kisiasa, kisheria, diplomasia ya umma, na vyombo vya habari kwa lengo la kuutenga utawala wa dhuluma wa Israel," waandaaji walisema katika taarifa yao.
Mkutano huo utakuwa na mijadala na warsha kadhaa. Wazungumzaji ni pamoja na Declan Kearney, mwenyekiti wa Sinn Fein; Mustafa Barghouti, kiongozi wa Mpango wa Kitaifa wa Palestina; na Mchungaji Munther Isaka kutoka Bethlehemu.