Lido Abdikarin Abdille anaishi kaskazini mwa Somalia, akikabiliana na misukosoku ya maisha na kupigwa na ukame usioisha unaosababisha hasara ya karibu nusu ya mifugo yake tangu mwaka 2020.
"Tunategemea mifugo kwa kila kitu. Ikiwa mnyama anaweza kuwa dhaifu, kama inavyotokea wakati wa ukame ambapo ng'ombe hawana chakula, huwezi hata kumnyonyesha," anasema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 34.
Tangu baba yake alipofariki mwaka 2010, Abdille amekuwa na jukumu la kumuuguza mama yake na kuwalea watoto wake wawili katika Jimbo la Puntland nchini Somalia. Maisha yamekua magumu kufuatia mabadiliko ya hali ya hewa, kwanza ukame wa muda mrefu na kisha mafuriko yaliyokua kwa muda mrefu.
Ingawaje hakua pekee yake katika mateso yake.
Zaidi ya mifugo milioni 13.2 katika eneo la Pembe ya Afrika ilipotea wakati wa ukame wa 2020-2023, ambao umeelezwa kama mbaya zaidi katika miaka 40.
Takwimu kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Shirika la Chakula na Kilimo zinaonyesha kuwa Ethiopia ilipoteza zaidi ya mifugo milioni 6.8 kutokana na ukama mabaya.
Nchini Somalia, idadi ilikuwa takriban milioni 3.8. Kenya nayo ilipoteza zaidi ya ng'ombe milioni 2.6.
Dk Mohammed Guleid, mtaalam wa maisha katika eneo kame la Pembe ya Afrika, anaorodhesha ukame huo kuwa kati ya majanga ya asili yenye madhara makubwa kutokea.
"Na kisha ikaja mvua inayosababishwa na El Niño na mafuriko kuuwa kilichosalia," akiambia TRT Afrika.
Kaskazini mwa Somalia, Abdille na wakulima wengine na wafugaji walikuwa bado wanapambana kurudi kutokana na miaka mitatu ya ukame wakati mvua ilipoanza kwa ghadhabu, nyumba zikasombwa, na zaidi ya watu 100 kufa.
Mfululizo wa haraka wa ukame na mafuriko uliwapeleka Abdille na wafugaji wengine mamilioni kwenye ukingo wa njaa na uharibifu wa kiuchumi.
Suluhisho la bima
Huku mahitaji ya suluhisho la kuokoa maisha na riziki mbele ya matukio ya hali ya hewa kali yanazidi kuwa wazi, mpango wa bima ya mifugo ulitolewa hivi karibuni nchini Somalia.
Bima ya Mifugo kulingana na Kiashiria (IBLI) inalenga kulinda jamii dhidi ya mshtuko wa ukame kwa kutoa malipo wakati wafugaji wanapoteza wanyama kutokana na maafa ya hali ya hewa.
"Bima hii, kwa njia moja, inawawezesha wafugaji hivyo wasiwe waathirika wa hali ambazo ziko mbali na udhibiti wao," anasema Dk Guleid.
Utafiti wa mwaka 2018 na Shirika la Maendeleo la Marekani ulihesabu kuwa dola 1 ya marekani ukifika kwa wakati unalingana na dola 3 ya Marekani katika matumizi ya kibinadamu baadaye.
Hii inamaanisha msaada uliocheleweshwa na gharama za kurudisha mifugo ni mara tatu zaidi ya kuendelea kuwawezesha wanyama kuishi kupitia ukame kwa kununua chakula.
"Njia hii inafanya kazi kupitia picha za malisho zinazochukuliwa kupitia satelaiti wakati wa ukame. Wameunda vigezo wanavyoweza kuona kiwango cha malisho kwa asilimia kupitia satelaiti. Hivyo, mara malisho yanapofikia asilimia fulani, wanachukua hatua kwa kusaidia wafugaji," anaeleza Dk Guleid.
Washiriki hupokea fidia kwa kuchangia kiwango kinacholingana na ukubwa wa kundi la mifugo walio katiwa bima.
Abdille ni mmoja wa Wasomali 40,000 waliojisajili katika mpango huo tangu Agosti 2022 na kupokea malipo ya dola 50. "Fedha hizi zitasaidia katika maisha yetu na mifugo. Tunaweza kununua majani na maji wakati wa ukame, kuokoa ng'ombe, mbuzi, na ngamia wetu," anasema.
Muusa Ali Mahamad, mkurugenzi wa mawasiliano wa Benki ya Salaam Somali, mmoja wa wadhamini wa mradi huo, anasema hii ndio bima ya kwanza iliyoundwa kwa wafugaji wa Kisomali.
Uhamiaji wa kulazimishwa
Abdifatah Jama Hassan, pia kutoka Puntland, anabainisha kwamba wengi kama yeye wamelazimika kuhamia mijini kwa ajili ya kazi baada ya kupoteza riziki yao ya asili kwa sababa ya ukame.
"Nchi yetu inakumbwa na ukame mara kwa mara, na hali ya hewa haitabiriki. Njia ya asili ya maisha ya wafugaji haitoshi tena," anasema Abdifatah mwenye umri wa miaka 43.
Mpango wa bima ni mwangaza baada ya huzuni wa muda. "Hii ni kitu kipya kabisa kwa wafugaji wa Kisomali, lakini tayari tunaweza kuhisi faida tunazopata zinazidi kiasi kidogo cha pesa tunacholipa kwa bima," akihadithia TRT Afrika.
Ufadhili wa kifedha umemtia moyo mbele ya tishio la mara kwa mara la ukame.
"Naamini kuwa hii itachochea watu wasiache kufuga wanyama... Hata katika ukame mbaya, bado kutakuwa na njia ya kuokoa wanyama," anasema Abdirizak Hussein Mohamed, mwenye umri wa miaka 39.
Lakini hata wakati hakuna tishio la papo hapo la mafuriko au ukame, mifugo bado inakabiliwa na mambo mengine.
"Mabadiliko ya hali ya hewa na magonjwa daima wanawatishia, na kwa kiwango kidogo, wanyama pori. Wanakabiliwa na hatari wakati wowote," anasisitiza Dk Guleid.
Biashara yenye faida
Hata hivyo, licha ya utata wa sekta ya mifugo, inaweza kuwa chanzo chenye faida cha riziki kwa familia na chanzo cha mapato kwa nchi.
"Biashara ya mifugo ina minyororo mitatu ya thamani - nyama, maziwa, na ngozi," Dk Guleid anaeleza TRT Afrika.
Mara nyingi kuna soko tayari kwa bidhaa nyingi, kitaifa na kimataifa.
"Kilo moja ya nyama ni karibu shilingi 1,000, chini kidogo ya dola 10 za Marekani. Hakuna nafaka inayokupa shilingi 1,000 kwa kilogramu. Na kuna mahitaji makubwa ya nyama, haswa kutoka Mashariki ya Kati. Kwa bahati mbaya, biashara haitoshi," anasema Dk Guleid.
Nchini Kenya, serikali inaandaa mpango wa mifugo ili kusaidia kutengeneza sera itakayosababisha utumiaji bora wa rasilimali.
Hatua sahihi za kupunguza hasara zinazosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa zikichukuliwa, uwezekano wa kukuza sekta ya mifugo barani Afrika ni mkubwa.
Botswana inasifiwa kua mfano bora katika bara la Afrika kwa mazoea bora katika usimamizi wa mifugo.
Kurudi Somalia, Dk Guleid anashuhudia kuwa jamii lazima ihimizwe kufanya biashara ya ufugaji wa mifugo kibiashara ili kufaidika kabisa.