Msemaji wa serikali ya Comoro amongelea kuhusu maneno makali yaliyotumiwa na afisa wa Ufaransa siku ya Alhamisi katika kipindi cha televisheni Ufaransa juu ya wahamiaji kutoka Comoro.
Katika mahojiano maalum na TRT Afrika, Houmed Msaidie, Msemaji wa Serikali ya Comoro, alipokea kwa masikitiko makubwa tangazo la afisa huyo mteule wa Ufaransa anayetaka mauaji ya wahamiaji kutoka Comoro.
“Kauli yake inaonesha chuki na kauli hii hailingani na nafasi aliyonayo. Tungependa kuimarisha mahusiano kati yetu na pia ushirikiano kati ya nchi hizi mbili, ila sio kwa njia hii.” alisema Bw. Houmed Msaidiye.
Kauli hii kutoka Comoro inakuja siku nne baada ya Salime Mdere, makamu wa rais wa Bunge la Kisiwa cha Mayotte, eneo la ng'ambo ya Ufaransa, kutoa wito wa mauaji ya wahamiaji kutoka kisiwa cha Afrika Mashariki cha Comoro, na maafisa wa sheria.
Akizungumza kwenye kituo cha utangazaji cha Ufaransa, France 1, kuhusiana na mpango wa Ufaransa wa kuwatimua wahamiaji haramu katika kisiwa cha Bahari ya Hindi, Mdere aliwaita Wacomoria waliopinga operesheni hiyo kuwa ni magaidi.
"Napima maneno yangu, wengine wauawe ikibidi, tusipomuua mmoja, wengine watakuwa na ujasiri na wengine watataka kuua polisi," Mdere alisema na kueleza kuwa polisi wanaweza kuwaua wahamiaji hao ili kujilinda.
Msemaji wa serikali aeleza kuwa "Takriban 80% ya Wacomoro wanaokwenda Mayotte hawana haja ya kuishia huko kwa sababu nchi ni maskini kuliko sisi. Uwa wanaelekea Paris, Marseille, Reunion na kwingineko. Malengo yao ni kwenda Ufaransa kwa sababu nchi hii imetutawala kwa zaidi ya miaka 150."
"Ufaransa haipaswi kutishia maisha ya watu wetu. Waliondoka na mali zetu." aongeza Msaidie.
Napima maneno yangu, wengine wauawe ikibidi, tusipomuua mmoja, wengine watakuwa na ujasiri na wengine watataka kuua polisi
Kwa mujibu wa sheria za Ufaransa, mtumishi wa umma anayetoa matamshi ya uchochezi, vitisho au chuki katika eneo la umma anapaswa kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu hadi mitano jela na atatozwa faini ya hadi karibu dola 50,000 (Euro 45,000).