Rais wa zamani wa Nigeria, Goodluck Jonathan, ndiye anayeongoza ujumbe huo wa Baraza la Wazee wa Afrika Magharibi (WAEF), linalotarajiwa kuongoza uangalizi wa uchaguzi huo Monrovia.
Aidha, ujumbe huo pia unamshirikisha pamoja na waziri mkuu wa zamani wa Burkina Faso na Rais wa wakati mmoja wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS), Kadre Ouedraogo.
"Timu itakuwa tayari kuchunguza jinsi uchaguzi utakavyoendelea kutoa msaada wao kuhakikisha uchaguzi wa amani na kuimarisha demokrasia nchini, kwa kutumia uzoefu wao kama viongozi wa zamani wa ukanda huo."
Aidha, watatembelea vituo vya kupiga kura vya Monrovia, Liberia ili kukagua taratibu za siku ya uchaguzi na mchakato wa kukusanya matokeo na kubaki kushiriki hadi matokeo yatakapotangazwa.
Wajumbe hao wa ujumbe wa WAEF wanatarajiwa kuwa nchini Liberia kwa takriban siku kumi.