Donald Trump anaonekana kujiamini kufuatia kampeni zake./Picha: AP

Ulinzi mkali ulitawala maeneo mengi nchini Marekani huku mamilioni ya wapiga kura nchini humo wakichamgua Rais wa 47 wa nchi hiyo siku ya Jumanne.

Makamu wa Rais Kamala Harris na mgombea wa chama cha Republican Donald Trump wanachuana vikali katika uchaguzi huo, huku tafiti mbalimbali zikionesha tofauti ndogo kati yao.

Iwapo atashinda uchaguzi huo, Trump atakuwa Rais wa kwanza kushika madaraka baada ya kushitakiwa kwa makosa mbalimbali ya uhalifu.

Pia, atakuwa Rais wa pili kwenye historia ya nchi hiyo kushinda nafasi ya Urais kwa awamu tofauti, baada ya Grover Cleveland kufanya hivyo katika karne ya 19.

Kwa upande wake, Harris anasaka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika na Asia Kusini kuwa kiongozi wa nchi hiyo.

Ulinzi mkali umeimarishwa kwenye vituo vya kupigia na kuhesabia kura nchini humo, huku maofisa usalama zaidi wakiongezwa maeneo mbalimbali ili kuimarisha ulinzi.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

TRT Afrika