Uchaguzi huo utawakutanisha Makamu wa Rais Kamala Harris dhidi ya Donald Trump. /Picha: DPA / Picha: Reuters  

By Mazhun Idris

TRT Afrika, Istanbul, Uturuki

Tofauti na uchaguzi iliopita, Uchaguzi wa Marekani kwa mwaka 2024 umetawaliwa na kimuhemuhe kikubwa, kama anavyosema Nicole, mmarekani mweuzi kutoka jimbo la Wisconsin.

"Hali ya shinikizo ipo juu, hata kwenye mitandao ya kijamii," anasema mhitimu huyo kutoka Chuo Kikuu cha Wisconsin Madison.

Kwa Nicole, ni bora tu "uchaguzi huo uishe mapema."

"Hali ilivyo kwa sasa"

Nicole anaonesha wasiwasi wake kama mwanamke mweusi nchini humo.

Hali hiyo inaashiria hisia za wapiga kura wengi wenye asili ya Kiafrika nchini humo.

Sintofahamu hiyo kati ya wapiga kura wenye asili ya Kiafrika si kitu kipya, haswa kwa kuwa wagombea hao wawili wamebeba siri kuu ya Marekani na watu wake.

Uchaguzi wa Novemba 5 unakuwa ni wa 60 kwenye historia ya nchi hiyo. Mamilioni ya wapiga watamchagua Rais na Makamu wa Rais kwa kipindi cha miaka nne, kitakachoanza Januari 2025.

Kura za mapema

Wagombea hao watakuwa wanasaka fursa ya kuchukua nafasi ya Joe Biden, Makamu wa Rais kutoka chama cha Demorat ambaye alijiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho mwezi Julai.

Kamala Harris anagombea kiti hicho kwa tiketi ya Demokrat akiwa na mgombea mwenza wake Tim Walz, ambaye ni gavana wa Minnesota.

Donald Trump, ambaye ni Rais wa 45 wa Marekani alishindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2021, amemsimamisha James David Vance, seneta wa Ohio kama mgombea wake mwenza.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 75 tayari wamepiga kura nchini humo.

Tafiti tofauti, zinaonesha kuwa kutakuwa na mtifuano mkali kati ya Harris na Trump.

Licha ya wito wa kushiriki kwenye uchaguzi huo, bado kuna hofu ya jamii za watu weusi kulengwa hata baada ya mchakato mzima.

Nicole anahofu kuwa itambidi aridhike tu na maoni ya watu kuhusu ubaguzi wa rangi, hasa baada ya uchaguzi huo.

Hata hivyo, bado anaonesha imani yake kwenye uchaguzi huo.

'Mgombea wa wote'

"Ni imani yangu kuwa kila mmoja inabidi ajiandikishe kwa ajili ya kupiga kura kwa ajili ya mgombea si tu atakayewasaidia, bali atakayewasaidia na majirani zao," anasema Nicole.

Takwimu zinaonesha kuwa kuna idadi kubwa ya watu weusi wanaopiga kura ukilinganisha na jamii za Walatino na za Waasia. Mwaka 2024, idadi ya wapiga kura wenye asili ya kiafrika itaongezeka na kufikia milioni 34.4, ambayo ni nyongeza ya asilima 7 kutoka mwaka 2020.

Hii ndio sababu inayowafanya wapiga kura weusi kuwa na ushawishi mkubwa kwenye matokeo ya uchaguzi huo.

Kwa miaka mingi sasa, uchaguzi wa Marekani umevikutanisha vyama vya Demokrat na Republican, huku masuala mbalimbali kama vile uchumi, huduma za afya, uhamiaji, sheria na mageuzi kwenye kodi yakitawala mchakato huo.

Mivutano ya kimataifa

Uchaguzi wa mwaka huu unapigiwa chapuo zaidi kutokana na vita vinavyoendelea nchini Ukraine na Mashariki ya Kati.

Chini ya Biden na Harris, Washington imesisitiza kuiunga mkono Ukraine, huku pia ikuinga mkono ukatili unaofanywa dhidi ya watu wa Palestina na Israeli.

Ndani ya nchi, Wamarekani weusi hawatosahau kamwe historia yao ya mapambano ya kikatiba na kijamii kuhusu haki za kupiga kura.

Hii ni jamii ambayo haijawahi kuridhika kwenye masuala ya haki ya kupiga kura, tangu kuanzishwa kwa taifa hilo.

Kikatiba, haki ya kisheria kwa raia wote wa Amerika ilifafanuliwa kwanza mnamo 1870.

Hata hivyo, iliichukua nchi hiyo marekebisho kadhaa ya kikatiba na hatua ya Congress kuongeza haki za kupiga kura kwa raia wa wenye asili ya Kiafrika wa jinsi zote.

Harris anawania nafasi ya kuwa Rais wa kwanza mwanamke wa Marekani.

Kwa upande mwingine, ushindi wa Trump utamaanisha kuwa rais wa kwanza wa zamani kushinda baada ya kupoteza fursa hiyo.

TRT Afrika