Nigeria Tiwa Savage / Photo: AP

Msanii maarufu wa muziki wa Afro Beat Tiwa Savage amethibitisha kuwa wahalifu walivamia nyumbani kwake.

Kupitia barua rasmi ambayo imechapishwa katika ukurasa wa Tiwa Savage wa mtandao wa Instagram uongozi wa msanii huyo umeandika kuwa kulikua na ukiukwaji mkubwa wa usalama nyumbani kwa msanii huyo.

"Kufuatia ripoti za hivi majuzi mtandaoni, tunaweza kuthibitisha kwamba Alhamisi tarehe 13 Aprili 2023 kulikuwa na ukiukaji mkubwa wa usalama katika makazi ya mwanamuziki Tiwa Savage" ilithibitisha taarifa hiyo

Hata hivyo bila kufafanua nini hasa kilicho tokea, taarifa hiyo imethibitisha kuwa msanii huyo na familia yake wapo salama na wahalifu waliohusika wamekamatwa.

"Idadi ya washukiwa walikamatwa na kwa sasa wanazuiliwa chini ya uchunguzi katika Kituo cha Polisi cha Alagbon, Ikoyi".

"Bi Savage na familia yake wako salama na wanaendelea vyema", taarifa hiyo iliongeza

Kupitia mitandao mbali mbali ya kijamii wafuasi wa msanii huyo wameendelea kutuma salamu za pole na kumtakia heri msanii huyo wa kike mashuhuri kutoka Nigeria.

TRT Afrika