NBA Africa inasema kilabu cha Dynamo kimekaata kufuata sheria za Mpira wa Kikapu Afrika/ picha kutoka NBA Africa  

Mabingwa wa Burundi wa Mpira wa kikapu, basketball, Dynamo wamejiondoa kwenye Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (BAL) 2024 .

"Kilabu cha Dynamo kimekaata kufuata sheria za Mpira wa Kikapu Afrika , National Basketball Africa, zinazohusiana na sare za michezo." taarifa kutoka kwa rais wa NBA Africa Amadou Gallo Fall imesema, " na hapo kukosa kucheza kwa mchezo ya leo na Petro De luanda ya Angola na kuhusiaka katika msimu wa 2024 wa NBA."

Hii ni baada ya kukataa kwa mara ya pili kuvaa sare za kuonyesha nembo ya "Visit Rwanda" kwenye jezi zao.

#VisitRwanda ni mmoja wa washirika wakuu wa mashindano ya bara.

Chini ya sheria za FINBA kukosa michezo miwili katika michezo ya msimu moja inalazimisha timu kuondoka katiak michezo.

Rwanda na Burundi zina mvutano wa kisiasa kati yao ambao inatishia kuvunja uhsuiano kati yao, ikiwa Burundi inadai kuwa Rwandsa inaunga mkono waasi wanaoishambulia, jambo amablo serikali ya Rwanda imekataa.

TRT Afrika