Watu wapatao 16 walipoteza maisha kufuatia kuporomoka kwa jengo la biashara siku ya Novemba 16, 2024 jijini Dare es Salaam./Picha:Wengine

Vikosi vya uokoaji vimeendelea kuchimbua vifusi kwa siku ya nne mfululizo, wakiendelea kuwatafuta manusura wa tukio la Novemba 16 ambalo limsababisha vifo vya watu 16 hadi kufikia sasa.

Jengo hilo la ghorofa 4, liliporomoka mapema Jumamosi, wakati baadhi ya wafanyabishara wa eneo hilo wakiwa wanajiandaa kuanza na shughuli zao za kila siku.

Kulingana na serikali ya Tanzania, watu 88 wameshaokolewa hadi kufukia sasa huku wengine wakihofiwa kuwa bado wako chini ya vifusi vya jengo hilo.

Kulingana na Makoba, zoezi la uokoaji lilikuwa likiendelea kwa kasi inayotakiwa, tofauti na taarifa za awali kuwa lilikuwa likisuasua.

“Ni vigumu kwa watu ambao wako mbali na eneo la tukio kuelewa kinachoendelea hapa. Ni vigumu kutumia mashine kubwa kuondoa vifusi, hasa kutokana na namna jengo lilivyoporomoka…ni muhimu sana kulifanya kwa uangalifu ili kuepusha madhara zaidi,” alisema.

Kwa mujibu wa msemaji huyo, shimo maalumu ili waweze kuwasiliana na manusura hao huku wakiendelea kuwapa msaada wa oksijeni na maji.

Wakati huo huo, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu wa nchi hiyo Kassim Majaliwa kuongeza zoezi la uokoaji kwa saa 24 zaidi.

Agizo hilo linajiri saa 72 toka kuporomoka kwa jengo hilo, siku ya Novemba 16.

Rais Samia alitoa agizo kwa njia ya simu, akiwa Brazil ambako anahudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za G20.

TRT Afrika