Kenya Airways USA / Photo: AP

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA imeamua kubadilisha safari za Shirika la Ndege la Kenya-KQ kati ya Nairobi na Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 mwezi Januari. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Tanzania TCAA.

Taarifa hiyo, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu Hamza Johari, imesema, uamuzi huo umechukuliwa baada ya Mamlaka husika nchini Kenya kukataa ombi la Tanzania la kutaka ndege zake zote la mizigo kupitia Nairobi, hivyo kukiuka kifungu nambari 4 cha makubaliano ya anga yaliyotiwa saini tarehe 24 Novemba, 2016 kati ya Tanzania na Kenya.

“Kufuatia uamuzi huu, hakutakuwa na ndege za abiria kupitia KQ kati ya Nairobi na Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 Januari, 2024,” imesema taarifa hiyo.

TRT Afrika