Tanzania yatangaza mpango wa kujenga na  kurusha setelaiti yake angani. Picha: Ikulu Tanzania

Na Lulu Sanga

Kwa mara ya kwanza Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ameweka wazi mpango wa nchi hiyo kujenga na kurusha setelaiti yake angani ambayo itafanyikia nchini humo.

Rais huyo amezungumza hii leo wakati akiwa katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa minara ya kurusha matangazo ya Televisheni ardhini (DTT), ambapo amesema kuwa tayari mazungumzo yamekwisha anza.

"tunajipanga kuja na setelaiti ambayo niwahakikishie kuwa itakuwepo Tanzania, tunajipanga vizuri tumeanza mazungumzo tutajenga setelaiti Tanzania.” Rais Samia alibainisha

Mpango wa serikali ya Tanzania unawekwa wazi mwezi mmoja tu tangu kurushwa kwa setelaiti ya nchi jirani ya Kenya.

Ikiwa Tanzania itafanikisha hatua hiyo kubwa katika ulimwengu wa tekinolojia, itakuwa ni miongoni mwa nchi chache za Afrika zilizofanikisha kupeleka kifaa hicho angani yaani Algeria, Ethiopia, Kenya, Zimbabwe, Afrika Kusini, Morocco, Misri, Ghana na Nigeria

TRT Afrika