Sehemu ya Treni inayotumia umeme iliyofanyiwa majaribio na TRC./Picha:TRTAfrika

Shirika la Reli Tanzania(TRC) limeanzisha safari ya majaribio ya treni yenye kutumia nishati ya umeme (SGR) kutoka mkoa wa Dar es Salaam hadi Morogoro.

Hii ni sehemu ya serikali ya Tanzania ya kuleta mapinduzi kwenye njia hii ya usafiri, kongwe zaidi nchini humo.

Malengo ya mradi ni kupunguza gharama za usafiri, kupunguza muda wa kusafiri, ufikiaji rahisi kwa huduma mbalimbali za jamii kwa jumuiya ya eneo la mradi na uwezeshaji wa biashara kati ya Tanzania na nchi za jirani.

Njia hii ya reli pia inalenga kurahisisha usafiri wa bidhaa kati ya bandari ya Dar es Salaam na miji ya Kigali, nchini Rwanda na baadaye Bujumbura, Burundi, na Goma, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ujenzi wa mradi wa SGR ulianza Aprili 2017 ambapo awamu ya kwanza, ujenzi ulianzia Dar es Salaam mpaka Morogoro kwa umbali wa kilometa 300.

Reli hiyo inaanzia katika bandari ya Bahari ya Hindi, Dar es Salaam hadi katika pwani ya Mwanza kwenye Ziwa Victoria ili kuunganisha nchi jirani.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa TRC Masanja Kadogosa, Tanzania imeazimia kutumia SGR kama mbadala wa njia za reli za kawaida ambazo zilianza kutumika wakati shirika hilo likiwa ni sehemu ya Shirika la Reli la Afrika Mashariki.

Mara baada ya kuanza kutumika Julai 2024, treni za SGR, zitakuwa zinasafiri kwa kasi ya wastani wa kilomita 160 kwa saa, na hivyo kupunguza kwa saa nne, safari za mabasi kati ya Dar es Salaam na Morogorokati ya Dar na Morogoro na saa tano zinazotumika na reli ya zamani.

TRT Afrika