Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan./Picha: X

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameunda kamati maalumu ya kutathmini na kushauri kuhusu masuala ya kodi nchini humo.

Uamuzi huo, unalenga kutatua changamoto wanazokutana nazo wafanyabiashara zikiwamo kufungiwa akaunti za benki, kuchukuliwa fedha bila utaratibu sahihi na kufungiwa mashine za kutoa risiti (EFD).

Tume hiyo ya watu 8, pia inawahusisha wataalamu wa uchumi, akiwemo aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Florens Luoga, na Mdibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini humo, Prof Mussa Juma Assad.

Pia yumo aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato wa Tanzania (TRA) Rished Bade.

Idadi kubwa ya wafanyabiashara nchini Tanzania wamelalamikia changamoto cha mashine za EFD./Picha:X 
TRT Afrika