Wengi wa watu waliokimbia makazi yao wanakimbilia nchi jirani ya Chad        

Takriban watu 700 waliripotiwa kuuawa huko Darfur Magharibi baada ya mapigano kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Rapid Support Forces (RSF), Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) lilisema katika taarifa.

Shirika hili limesema watu 100 walijeruhiwa na wengine 300 waliripotiwa kutoweka kufuatia mapigano huko El Geneina mnamo Novemba tarehe 4 na 5.

Wengi wa watu waliokimbia makaazi yao wanakimbilia nchi jirani ya Chad.

Mapigano ya silaha kati ya jeshi la Sudan na RSF yalianza mwezi Aprili juu ya mzozo wa madaraka.

Maelfu ya watu wameuawa kote nchini na mamilioni ya wengine kuyahama makaazi yao.

Katika mazungumzo huko Jeddah, pande zinazozozana zilikubali kuwezesha uwasilishaji wa misaada na hatua za kujenga imani, wapatanishi walisema Jumanne, lakini juhudi za kupata usitishaji mapigano hadi sasa zimeshindwa.

TRT Afrika