Na Charles Mgbolu
Sekunde chache tu inatosha kukunasa na kuvutiwa na video za dansi za TikTok zenye mavazi ya kuvutia za Kiafrika, zikishangiliwa na umati wa watu wenye shangwe.
Katika video moja kama hiyo kwenye akaunti ya TikTok ya @Kru_Krou kutoka Liberia, wapiga ngoma wanaonekana wakipiga ngoma za asili za ngozi ya kondoo na gonga za chuma ili kupatanisha kinyago chenye kurukaruka ambacho hupigisha mguu wake kwa kuupinda kwa nguvu, na kufuatiwa na densi ya kasi. Mara kwa mara kuona manyoya yaliyowekwa kwenye kiuno chake yakitikisika kwa karibu kasi ya mwanga.
Katika hekaya za Kiafrika, vinyago huonwa kuwa kiwakilishi halisi cha miungu ya kitamaduni inayoabudiwa na wapenda utamaduni kwa sababu wao huaminiwa kuleta bahati nzuri kutoka katika makao ya roho.
‘’Mionekano ya kinyago ni safi na takatifu,’’ anasema Christopher Okereke, mwanamila wa jadi kutoka kusini-mashariki mwa Nigeria.
‘’Wanawageuza wanadamu waliovaa kuwa vitu visivyo vya kawaida. Wao ni msingi wa utamaduni wa Kiafrika na wanatutofautisha kama jamii kutoka kwa mataifa mengine duniani,’’ anaiambia TRT Afrika.
Lakini mitindo ya magharibi inatia doa haraka utamaduni huu, na vyombo hivi vitakatifu, vya kitamaduni vilivyowahi kuheshimiwa kama miungu wenyewe sasa vinaangaziwa kwenye majukwaa na mitandao ya kijamii kama vile TikTok, haswa kwa burudani.
Maoni ya mitandao ya kijamii
Vinyago vya kucheza kwenye TikTok sasa vimetazamwa na mamilioni na vinashirikiwa zaidi ya kurasa za kijamii za TikTok, na meme nyingi zinazotolewa kutoka kwa video.
‘’Utaona kinyago akinywa pombe hadharani au kuwa pamoja na wanawake wanaocheza ngoma. Binafsi, namwambia mtu yeyote anayejali kusikiliza kwamba hizi si vinyago vya kweli, kwa sababu hakuna kinyago cha kweli cha Kiafrika kitakachowahi kufanya hivi,'' Okereke anaiambia TRT Afrika.
Wasiwasi wake unaonekana kuwa halali, huku baadhi ya video zikivuta hisia kutokana na kejeli zinazokiuka mipaka y aimani —kutoka kwa vinyago kuwasujudia wanasiasa na kuomba pesa kwa wengine kwa kulewa na kujikwaa barabarani, wakidhihakiwa na wapita njia.
Baadhi ya video hizo zimeonyeshwa katika nia ya kutaka kutazamwa kwenye mitandao ya kijamii na imezua mjadala miongoni mwa wapenda utamaduni.
Wana wasiwasi kuhusu kama umuhimu mkubwa wa kitamaduni wa vinyago vya Kiafrika unafagiliwa mbali na mikondo yenye nguvu ya mitindo ya kisasa ya mitandao ya kijamii.
‘’Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba kizazi cha vijana kinaweza kukua na dhana hii kwamba hivi ndivyo kinyago cha Kiafrika kinapaswa kuwakilisha, lakini huu ni mtazamo potofu. Vinyago huwa havifanyi kwa sababu wanataka kukusanya maoni kwenye mitandao ya kijamii,’’ alisisitiza.
Hoja zake, hata hivyo, zinapingwa vikali na Patrick Adigwe, mbunifu wa maudhui ya kitamaduni kwenye Facebook.
‘’Utamaduni unaendana na wakati tuliopo sasa, na hii ni hakikisho salama kwamba utamaduni wetu kama Waafrika hautakufa kamwe kwa sababu unaunganishwa na nguvu ya mitandao ya kijamii,’’ Adigwe aliiambia TRT Afrika.
‘’Ni fursa ya kukutana na kizazi kijacho pale walipo, na hiyo ni kwenye mitandao ya kijamii. Tunapaswa kufurahi hii inazua udadisi wao.
Gen Zs (kizazi kipya) sasa wanauliza maswali na kujifunza zaidi kuhusu mizizi yao ya kitamaduni, ambayo labda hawakuwahi kujua kama si kwa mitandao ya kijamii.
''Masquerade hutimiza majukumu tofauti,'' anasema Okereke. ''Ndiyo, wanaweza kuburudisha, lakini lazima uwe mwangalifu usiwahi kutumia kinyago ambacho ni kwa ajili ya mazoezi ya kimsingi ya kiroho na kuvaa kinyago chake kucheza kwenye TikTok; hapa ndipo vijana wa TikTokers wanapokosea, na hili ndilo linalohitaji kurekebishwa haraka ili kulinda maadili yao ya kitamaduni,'' anahoji.
Hoja za kuunga mkono au kupinga masquarades kwenye Tiktok ni kitu cha kuchukuliwa kwa makini.
Kwa mwendelezo wa kitamaduni, kizazi kijacho lazima kipeperuke na kuchukua joho linalotangaza urithi wa Kiafrika, lakini watafanya hivyo ikiwa watazungumzwa kwa lugha wanayoelewa.
Hata hivyo, lazima wajifunze kwa uangalifu, kwani itakuwa bure kujaribu kuokoa nembo za kale ambazo hazina tena chembe ya umuhimu wa kitamaduni.