Niger, Burkina Faso na Mali wameunda muungano mpya wa ulinzi. Picha: Nyingine

Na Abdulwasiu Hassan

Hilo lilikuwa linatarajiwa kutokea kwa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) tangu Januari 28, wakati serikali za kijeshi za Mali, Burkina Faso na Niger zilipotangaza kujiondoa kutoka jumuiya hiyo.

Misukosuko yanaotarajiwa kutokea kufuatia kuundwa kwa muungano utakaoenda sambamba na nchi za Sahel yaonekana kufanikiwa, huku kukiwa na uwezekano wa kutibua misingi ya ECOWAS na kuwa na athari kubwa kwa utulivu wa kikanda.

Shirikisho hilo jipya sio tu kuhusu kundi la washiriki waanzilishi wa jumuiya hio ya kikanda iliyozaliwa mwaka wa 1975 kujitoa nje kwa hamaki.

Uhusiano kati ya ECOWAS na nchi tatu za Afrika Magharibi zinazotawaliwa na wanajeshi ulidorora mwaka jana baada ya Rais aliyeng'olewa madarakani wa Niger Mohamed Bazoum kupinduliwa katika mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Jenerali Abdourahamane Tchiani.

Mara tu baada ya mapinduzi, ECOWAS iliiwekea Niger vikwazo na kuonya kuhusu uwezekano wa kuingilia kijeshi ikiwa serikali iliyochaguliwa ya kiraia haitarejeshwa.

Viongozi wa kijeshi wa Mali na Burkina Faso, ambao pia walikuwa wamenyakua mamlaka kupitia mapinduzi ya kijeshi, walikuwa wepesi wa kusaidia utawala wa kijeshi wenzao nchini Niger.

Kwa pamoja, nchi hizo tatu ziliishutumu Ufaransa kwa kutumia ECOWAS kuwashambulia.

Kufikia mwanzoni mwa 2024, walikuwa wameamua kujiondoa kutoka kwa ujuimuiya hio yenye umri wa miaka 49.

Uhusiano kati ya ECOWAS na nchi tatu za Afrika Magharibi ulidorora mnamo 2023. /Picha: Wengine

ECOWAS ilijaribu kuzima mgogoro huo kwa kuondoa vikwazo iliyokuwa imeiwekea Niger na kujaribu kuzishawishi nchi hizo tatu zilizojitenga kurudi kwenye jumuiya.

Mnamo Julai 7, wakati viongozi hao wa kikanda walipokutana kwenye makao makuu yake huko Abuja nchini Nigeria kwa ajili ya mkutano wa 65 wa jumuiya hio, kulifahamika sababu ya kutokuwepo kwa Niger, Mali na Burkina Faso baada ya kutoa tangazo lao la pamoja siku iliyotangulia la mkataba wa kuanzisha Muungano wa L'Alliance des États du Sahel (AES).

Omar Touray, rais wa tume ya ECOWAS, alionyesha kusikitishwa baada ya kukataa kwa Mali, Burkina Faso na Niger kujiunga tena na jumuiya hio. Sio kwamba yeye au mtu mwingine yeyote anaweza kutarajia vinginevyo, kwa kuzingatia hali ya kutoridhika kwa nchi hizo tatu tangu mwaka jana.

Madhara

Wakati viongozi wa muungano wa Sahel wakionyesha hatua yao kama hatua iliyochukuliwa kwa maslahi ya watu wao, baadhi ya wachambuzi wanafikiri tofauti.

Msimamizi wa kijeshi wa Burkina Faso, Ibrahim Traore, alisema hatua alizochukua yeye na wakuu wenzake wa kijeshi zitaweka msingi wa "uhuru wa kweli, amani na maendeleo endelevu" ya nchi zao.

"Kanda ya AES ina uwezo mkubwa wa asili ambao, kama utatumiwa ipasavyo, utahakikisha mustakabali bora kwa watu wa Niger, Mali na Burkina Faso," alisema Traore.

Hata hivyo, baadhi wanaamini viongozi hao wa kijeshi hawana mamlaka ya watu wao kuchukua hatua kali kama kuziondoa nchi hizo tatu kutoka ECOWAS.

Sulaiman Dahiru, mwanadiplomasia mstaafu kutoka Nigeria, ni mmoja wa wale wanaoshikilia maoni hayo.

Baadhi wanahofia kwamba ushindani kati ya muungano mpya wa kijeshi na ECOWAS unaweza kupunguza mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi katika eneo hilo. /Picha: Getty

Balozi huyo wa zamani wa Nigeria anawaona viongozi wa kijeshi wa Mali, Burkina Faso na Niger wakijionyesha kama watu wenye nadharia ya idiyalisti na si wa riyalisti.

"Wanawatumbukiza watu wao katika mtafaruku wa kijamii na kiuchumi na kisiasa," anaiambia TRT Afrika.

Walakini, watu wa pande zote za mgawanyiko wanakubaliana kuwa shida hii itakuwa na athari kubwa.

Wakati wale walio upande wa AES wanafikiri mgogoro huo umelemaza jumuiya ya kikanda, wale waliobakia ECOWAS wanatumai kuwa nchi hizo tatu zitafikiria upya uamuzi wao mapema au baadaye.

Hali ya usalama

Moja ya hasara ya mgogoro ndani ya kanda hiyo ni usalama wa umma, ambao viongozi wa pande zote mbili wanadai kuupa kipaumbele.

Hata wakati nchi za eneo hilo zilipowekwa pamoja chini ya ECOWAS, bado zilijitahidi kuzuia hatari zinazotoka kwa majambazi na waasi.

Kulingana na wachambuzi, kuongezeka kwa pengo kati ya kambi inayojitenga na jumuiya hiyo kutawatia moyo zaidi majambazi na waasi ambao tayari wanafanya uharibifu katika eneo hilo.

Ikiwa kuna sababu yoyote ya kuwa na matumaini, nchi katika eneo hilo huenda zikatumia ushawishi wao wa pamoja kuokoa ECOWAS na kulinda maslahi yao ya pamoja.

"Kama wanachama waliobaki wa ECOWAS wanaweza kuunganisha rasilimali zao pamoja na kuongeza jeshi ili kukabiliana na hali tete, kitu chanya bado kinaweza kutokea," anasema Dahiru.

"Tatizo ni kwamba nyingi ya nchi hizi zina matatizo makubwa ya kifedha ya kukabiliana nayo."

Watu wengine wenye muono tofauti wanafikiri kwamba kujitenga kwa nchi hizo na ECOWAS kunaweza kutatiza biashara katika nchi zisizo na bandari kama Niger na Mali, kwani zinategemea nchi wanachama wa ECOWAS kusafirisha bidhaa kwa njia ya bahari.

"Nchi hizi zitateseka. Niger tayari ina tatizo katika kusafirisha mafuta yake kupitia Benin," Dahiru anaelezea.

ECOWAS imempa mamlaka Rais Bassirou Diomaye Faye wa Senegal na mwenzake wa Togo, Faure Gnassingbé, kuwashawishi watawala wa kijeshi wa Mali, Burkina Faso na Niger kujiunga tena na ECOWAS.

Ingawa hakuna mtu amekata tamaa kuwa mvutano huo hauwezi kusitishwa, mwaka uliopita umeonyesha kwamba itachukua zaidi ya diplomasia kupata suluhu.

TRT Afrika