Mapigano unaoendelea umeibua changamoto kubwa kwa mashirika ya kibinadamu kutoa msaada kwa njia salama, haswa na watu zaidi na zaidi wanaosonga, wakikimbia maisha yao, shirika la Umoja wa Mataifa lilisema.
Ikifafanua uamuzi wake, WFP ilielezea kuchukua hatua hiyo kwa sababu za kiusalama huku ikisema vita hivyo vimekuwa kikwazo kikubwa kwa juhudi za msaada wa kibinadamu nchini humo.
Aidha kudorora kwa usalama pia imewalazimu wafanyakazi wanaohusika kutoa msaada kwa zaidi ya watu 800,000, pamoja na wengi ambao walikuwa wamekimbia mapigano huko Khartoum.
"Mahali pa kukimbilia sasa umekuwa uwanja wa vita katika vita ambavyo tayari vimewaathiri sana raia," Eddie Rowe, mwakilishi wa WFP na Mkurugenzi wa Sudan amesema.
Mapema wiki hii, wahudumu wa kibinadamu waliripoti kwamba kazi zote za kambi hizo ndani ya Jimbo la Al Jazirah zilikuwa zimesimamishwa hadi taarifa zaidi kutokana na hali ya usalama.
"Tumejitolea kuwasaidia watu wa Sudan katika kipindi chao cha mahitaji makubwa, lakini usalama wa wafanyakazi wetu na washirika lazima uhakikishwe," Alisema Bwana Rowe.
Angalau takriban watu 250,000 wamekimbia jimbo hilo, kulingana na ripoti za awali kutoka kwa Shirika la kimataifa la Uhamiaji, IOM.
Wengi wamefurushwa kwa mara ya pili, baada ya kufika eneo hilo kufatia mapigano kuzuka katika mji mkuu wa Khartoum mapema mwaka huu.
Mbali na hayo, Mashirika ya misaada yamepunguza operesheni zao katika eneo la Wad Medani kutokana na mapigano huku wafanyakazi wakihamia nchi jirani wakiwa na matumaini ya kurudi mara moja hali ya usalama itakaporuhusu.