Umoja wa mataifa umekuwa ukilalamikia mashambulio yaliyo lenga mashirika ya misaada na uporaji wa ghala za chakula cha misaada yanayotihsia hali kuzorota zaidi Picha : Reuters

Mashirika ya misaada nchini Sudan yameonya kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa kali imefikia milioni 20, sawa na 40% ya wananchi wake.

Idadi hii imeongezeka kwa kasi zaidi ikilinganishwa na makadirio ya awali na kuongeza wasiwasi wa kutokea mkasa wa kibinadamu kwa kiwango kisichotabirika.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na mashirika na misaada na ya umoja wa mataifa maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni pamoja na mji mkuu Khartoum, mkoa wa magharibi wa Darfur, na sehemu za Kordofan, ambayo yote yameshuhudia mapigano, mashambulizi na uporaji tangu vita vilipozuka katikati ya mwezi wa Aprili.

Mapigano hayo yaliyozuka juu ya kung'ang'ania uongozi kati ya Jeshi la taifa na kikosi cha dharura cha RSF, yamesababisha zaidi ya watu milioni tatu kupoteza makazi yao huku wengine karibia milioni moja wakikimbilia nchi jirani.

Umoja wa mataifa umekuwa ukilalamikia mashambulio yaliyo lenga mashirika ya misaada na uporaji wa ghala za chakula cha misaada, jambo lililotishia wafanyakazi wao kutishia kukimbia kwa kuhofia maisha yao.

Mashirika hayo yanasema pia kuwa kukatizwa kwa njia za kupitisha misaada, kuhama kwa idadi ya watu, na uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na vita vyote vilichangia kuongezeka kwa njaa.

"Matokeo yanaonyesha ongezeko kubwa la kiwango kinachotarajiwa cha hali ya uhaba wa chakula," ripoti hiyo imesema, ikiongeza idadi inayokabiliwa na njaa kali na inayohitaji msaada wa haraka ilikuwa milioni 8.6 kuliko wakati kama huo mwaka jana.

Umoja wa Mataifa ulikuwa umetabiri hapo awali kuwa watu milioni 19.1 watakuwa na njaa ifikapo Agosti.

Wakulima waliambia Reuters kwamba kutokuwa na uwezo wao wa kupanda mazao kunaweza kuongeza kasi ya kuenea kwa njaa.

Reuters
TRT Afrika