Jenerali  Mohamed Hamdan Dagalo, 'Hemedti', aliyeibuka mtu mwenye nguvu Sudan, ni nani?

Jenerali  Mohamed Hamdan Dagalo, 'Hemedti', aliyeibuka mtu mwenye nguvu Sudan, ni nani?

Hemedti anaongoza kikosi cha RSF, kikosi cha kijeshi kinachoshutumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu
Hemedti aamuru RSF, kikosi cha kijeshi kinachoshutumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu

Mkuu wa Vikosi vya RSF Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo amefanya ziara yake ya kwanza nje ya Sudan tangu vita kati ya RSF na Jeshi la Sudan vilipoanza mwezi Aprili na kukutana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Tangu kuondolewa kwa Rais wa Muda mrefu wa Sudan Omar al-Bashir, Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, 'Hemedti' ameibuka kuwa mtu mwenye nguvu zaidi Nchini Sudan.

Dagalo, maarufu zaidi Kwa jina lake la Utani 'Hemedti', mwenye umri wa miaka 48, aliinuka kutoka kwa mfanyabiashara wa ngamia na kuwa kamanda wa kikosi cha kijeshi (RSF) akitaka kumwangusha mkuu wa Jeshi La Sudan Jenerali Abdel fattah al-Burhan.

Hemedti pia anajulikana kuhamisha uaminifu mara kwa mara kwani alishirikiana pamoja na Al-Burhan katika kumaliza utawala wa Rais wa muda mrefu wa Sudan, Al-Bashir (1989 2019).

Aidha, awali kufuatia amri ya Bashir, alimkamata kiongozi wa wanamgambo, Musa Hilal, ambaye alikuwa kibaraka cha serikali katika kupambana na waasi katika mkoa wa Darfur.

Hemedti, ambaye alibadilisha upande kulingana na masilahi yake mwenyewe, alifanya ushirikiano na nchi kadhaa na wakuu wa vita.

Hemedti baada ya kukutana na Rais Museveni, Picha: Kaguta Museveni X

Vikosi vyake viliripotiwa kuhusika katika mapigano ya Yemen na Libya.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alimpokea Hemedti jijini Moscow, siku hiyo hiyo alipozindua operesheni yake ya kijeshi dhidi ya Ukraine, mnamo Februari 24, 2022.

Hemedti pia aliwahi kupokelewa na viongozi kadhaa wa nchi za Kiarabu, pamoja na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi na Mwana wa Mfalme wa Milki za Kiarabu, Mohamed bin Zayed Al Nahyan.

Mtu mwenye mali zaidi

Hemedti alijikusanyia utajiri na mamlaka kwa kudhibiti maeneo mengi katika maeneo yenye madini mengi ya dhahabu huko Darfur.

Familia yake inamiliki kampuni ya madini ya dhahabu ya Al Junaid, iliyotekwa mnamo 2017 kutoka kwa Musa hilal, kiongozi wa zamani wa Wanamgambo wa Janjaweed.

Katika nchi ambayo mapato ya dhahabu yanachangia karibu 44% ya mauzo ya jumla, Hemedti na kikosi chake cha RSF wamejipa uhuru wa kifedha kutoka kwa jeshi la nchi hiyo.

Uhuru huu wa kifedha umeimarisha msimamo wa Hemedti na kumruhusu kuajiri makumi ya maelfu ya wapiganaji.

RSF, jeshi la wapiganaji ambalo linalaumiwa kwa makosa mengi ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika jimbo la Magharibi la Darfur na kwingineko, limekuwa jeshi ambalo halina silaha nzito na anga.

Hemedti alijikusanyia utajiri na mamlaka kwa kudhibiti maeneo mengi katika maeneo yenye madini mengi ya dhahabu huko Darfur. Picha: AFP

Hemedti ameinuka kutoka kuwa mfanyabiashara wa ngamia hadi kuwa naibu mkuu wa Baraza la mpito la uhuru lililoongozwa na Jenerali Al-Burhan.

Ufanisi muhimu zaidi, ni kupata uhuru wa RSF kutoka kwa jeshi, baada ya kuwa chini ya utawala wa moja kwa moja wa Al Bashir hapo zamani.

Hali hii imeisababisha Sudan kukamatwa katikati ya majeshi mawili: Vikosi vya silaha vya Sudan (SAF) vinavyoongozwa na Al-Burhan, na RSF inayoongozwa na Hemedti.

Hata hivyo, jeshi la Sudan SAF haikubali kuwepo kwa nguvu sambamba, hasa kwa kuwa tofauti kati ya Al-Burhan na Hemedti zimeonekana hadharani.

Marekebisho ya usalama wa kijeshi yanayofikiria "ushiriki kamili wa RSF katika jeshi" yaliwasilishwa kama sehemu ya mpango wa kipindi cha mpito cha miaka 2.

Hata hivyo, Hemedti amekataa kujumuisha majeshi yake katika jeshi la Sudan hadi baada ya miaka 10. Hatua ambayo inaonekana kama jaribio la kuimarisha RSF na kuifanya iwe na nguvu kuliko jeshi.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, watu wapatao 9,000 wameuawa katika ghasia nchini Sudan, lakini vikundi vya madaktari na wanaharakati wa eneo hilo wanasema idadi ya vifo huenda ikawa kubwa zaidi.

AA