Pande hizo mbili zinalaumiana kwa kuanzisha vita Aprili 15, baada ya wiki kadhaa za mvutano kuhusu kuunganishwa kwa wanajeshi wao katika kikosi kimoja/ Picha: Reuters 

Kikosi cha Dharura nchini Sudan kijulikanacho kama RSF kimeelezea nia yake y akuweka makubaliano ya kusitisha vita kwa muda mrefu na jeshi la taifa na kufungua njia za mashauriano ili kurejesha amani nchini humo.

Kauli hiyo imekuja wakati mapigano kati ya RSF na jeshi yakiingia katika wiki yake ya 20 bila upande wowote kupata ushindi huku mamilioni ya watu wakifukuzwa kutoka makwao katika mji mkuu na miji mingine.

Umoja wa Mataifa umeonya juu ya "janga la kibinadamu la idadi kubwa", na njaa inayoongezeka, kuporomoka kwa huduma za afya, na miundombinu iliyoharibika. RSF na wanamgambo washirika pia wameshutumiwa kwa mauaji ya kikabila huko Darfur Magharibi.

Pande hizo mbili zinalaumiana kwa kuanzisha vita Aprili 15, baada ya wiki kadhaa za mvutano kuhusu kuunganishwa kwa wanajeshi wao katika kikosi kimoja kama sehemu ya mpito kuelekea demokrasia.

Katik ataarifa kwa vyombo vya habari Jumapili Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo alionekana kuwa tayari kufanya mazungumzo na jeshi kuhusu sura ya taifa la baadaye la Sudan.

"Juhudi za kumaliza mgogoro huo wa muda mrefu lazima zielekezwe katika kufikia usitishaji vita wa kudumu, pamoja na masuluhisho ya kina ya kisiasa ambayo yanashughulikia vyanzo vya vita vya Sudan," ilisema taarifa hiyo.

Sudan mpya

Chini ya mpango wake wa "Sudan Reborn", Dagalo aliahidi kuwa RSF itafuata kanuni zilizopendekezwa awali kama vile utawala wa kitaifa unaojumlisha utawala wa kitamaduni, uchaguzi wa kidemokrasia na kuundwa kwa jeshi moja.

Kauli hiyo imekuja baada ya mkuu wa jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan kuwasili Jumapili huko Port Sudan katika safari yake ya kwanza nje ya mji mkuu tangu mapigano yazuke. Duru za serikali zinasema atasafiri hadi Saudi Arabia na Misri kwa mazungumzo.

Wapatanishi wa kikanda wameonekana kukubali hatua ya kujumlisha baadaye wanajeshi hao katika serikali ya mpito.

Reuters