Ethiopia Tigray  / Photo: AP

Shirika la chakula la Umoja wa mataifa WFP, limetangaza Jumanne kuwa litaendelea na utoaji msaada wa chakula eneo la Tigray nchini Ethiopia baada kusitisha zoezi hilo kwa muda wa miezi mitatu.

WFP ilichukua hatua hiyo ya kusitisha misaada kufuatia mashambulio dhidi ya wafanyakazi wake na uporaji wa misaada katika maghala.

Mashambulio hayo dhidi ya wafanyakazi wa mashirika ya misaada yaliripotiwa mara kadhaa ikiwemo mashambulio dhidi ya madaktari waliokuwa na mipaka na magari ya huduma ya dharura na vifaa vyao.

"Ugawaji wa misaada wa majaribio unaendelea katika vituo saba vya usambazaji wa chakula ambapo WFP na washirika wamekamilisha kulenga wanaohitaji misaada na kuwasajili kidijitali," taarifa kutoka kwa WFP ilisema.

WFP ilisitisha misaada yake eneo la Tigray mwezi Mei, lakini kufikia Juni, wakasitisha katika eneo zima la Ethiopia.

Zaidi ya watu milioni 20 wanahitaji msaada wa chakula nchini Ethiopia, taifa la pili barani Afrika lenye watu wengi, kutokana na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika Pembe ya Afrika katika miongo kadhaa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili.

TRT Afrika
Reuters