Sherehe kubwa ilifanyika katika ikulu ya rais jijini Mogadishu kuadhimisha miaka 63 ya siku ya uhuru wa Somalia.
Rais Hassan Sheikh Mohamud alishiriki katika sherehe ya kupandisha bendera ya maadhimisho ya uhuru wa mikoa ya Kusini mwa nchi na umoja wa Kaskazini na Kusini, kwa mujibu wa itifaki ya usiku wa uhuru na umoja mnamo Julai 1, 1960.
Rais Mohamud pia akiweka maua kwenye mnara wa Daljirka Dahsoon kuadhimisha miaka 63 ya uhuru na muungano wa Somalia.
Ujumbe wa heri
Umoja wa Mataifa inathibitisha tena kuunga mkono na Somalia ili kuhakikisha Somalia yenye umoja, amani na ustawi," alisema Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Catriona Laing.
"Ninawatakia wananchi na serikali ya Somalia furaha ya miaka 63 ya Uhuru!" Workeneh Gebeyehu, mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya maendeleo ya IGAD amesema, " Kama IGAD tunaungana nanyi katika kusherehekea siku hii ya kihistoria, Sote tushikane mikono kujenga mustakabali mzuri wa eneo letu kwa pamoja."
Ujumbe wa mpito wa Afrika nchini Somalia, ATMIS pia nayo imetoa ujumbe wake kupitia mitandao.
"Tunasherehekea uthabiti wa Somalia ya kujenga nchi salama, tulivu, yenye amani na ustawi."