Siku ya Alhamisi, Baraza la mawaziri la Somalia liliidhinisha muswada, ambao iwapo utaidhinishwa na bunge, utarejesha mfumo wa uchaguzi wa nchi hiyo kuwa wa upigaji kura.
Hii itakomesha mchakato wa upigaji kura usio wa moja kwa moja, msemaji wa serikali alisema.
Huku kukiwa na ukosefu wa usalama uliosababishwa na waasi na miundo dhaifu ya serikali.
Katika miaka ya hivi karibuni, wabunge walimpigia kura rais, huku wakuu wa koo na wazee wakiwachagua wabunge katika serikali ya shirikisho na majimbo ya kikanda.
Hapo awali nchi hiyo ilikuwa imepanga kupiga kura ya moja kwa moja mnamo 2020, lakini mizozo ya muda mrefu kati ya wanasiasa na ukosefu wa usalama unaoendelea kote nchini ulilazimisha kubakia na kura isiyo ya moja kwa moja.
"Sheria za uchaguzi zitaongoza nchi kwa mtu mmoja kura moja kitaifa," msemaji wa serikali Farhan Jimale alisema katika taarifa.
“Hii itawapa wananchi mamlaka ya kupiga kura na kuchagua kwa mara ya kwanza baada ya miaka 55. Ni siku ya kihistoria” alisema.
Sera hiyo ilitangazwa mwaka jana na Rais Hassan Sheikh Mohamud, ambaye alichaguliwa na wabunge kwa muda wa miaka mitano Mei 2022.
Utekelezaji wake unakabiliwa na changamoto kubwa za vifaa na usalama kwa sababu ya ukosefu wa miundombinu na al Shabaab, kikundi cha wanamgambo kinaendelea kudhibiti maeneo makubwa ya nchi.