Meya wa Zeytinburnu aliamua kubadilisha eneo hilo na kuwa makumbusho yenye kuonesha ugunduzi wa mabaki ya kale. Picha: Cemal Emden  

Na

Meryem Demirhan

Mara zote zoezi la uchimbaji linapofanyika Istanbul, ni vigumu kukutana na chembechembe za ustaarabu na usasa kwa chini.

Haishangazi, kuona uvumbuzi wa hivi karibuni katika wilaya ya Zeytinburnu huko Istanbul ukiibua furaha.

"Tunafahamu kuwa Istanbul ni sehemu yenye historia nyingi, lakini hii ndiyo ya kwanza ambayo tumegundua nje ya kuta za jiji. Na inatujaza msisimko mkubwa, kwani inaashiria nyongeza mpya kwa historia ya kipekee ya Istanbul, ikitoa ushahidi mpya wa siku zake za nyuma,” alisema Omer Arisoy, Meya wa Zeytinburnu na naibu waziri wa zamani wa Utamaduni na Utalii.

Mara zote zoezi la uchimbaji linapofanyika Istanbul, ni vigumu kukutana na chembechembe za ustaarabu na usasa kwa chini.

Mabaki hayo yalipatikana wakati wa urekebishwaji wa majengo ya enzi za Ottoman, ilipo ofisi ya manispaa ya Zeytinburnu kwa miaka 25 sasa. Kazi ya kuimarisha na kurekebisha miundombinu hiyo ilianza mwaka 2015 na wazo la kubadilisha jengo hilo la kihistoria kuwa kituo cha sanaa, na kuitwa kitua cha sanaa cha Kazlicesme.

Wakati wa ukarabati huo, Safu za sakafu, za zamani za Kirumi na Byzantine, ziligundulika chini ya jengo hilo.

Sehemu ya michoro iliyogundulika.

Kulingana na mifumo kwenye michoro, iliamuliwa kufanyika kwa uchunguzi wa nje wa jengo ili kujua iwapo ugunduzi huo umeenea kwa sehemu kubwa zaidi.

Utafutaji wa wataaalamu wa mambo kale ulizaa matunda, kwa kubaini kuwa michoro mingi ilipatikana ikiwa wazi, hadi kufikia 2019.

“Pamoja na vitu vingine, tumegundua michoro yenye ukubwa wa mita za mraba 186,” Arisoy aliongeza.

Kielelezo hiki kinaonesha baadhi ya michoro inayopatikana ndani ya jengo hilo la kihistoria.

Kadiri uchimbaji unavyoendelea, ndivyo msururu wa vitu vya kale vya kihistoria ambavyo havikutarajiwa unavyoibuka, na kuongeza tabaka za utajiri usiotarajiwa.

"Baada ya michoro hiyo kupatikana ndani ya jengo hilo, tuliifuata hadi mwisho wake na kufikia jiwe la kaburi, lililokuwa na mabaki ya mifupa ya watu wawili, mwanamume na mwanamke. Kulingana vipimo vya kaboni 14 na Tubitak, jiwe hilo lilianza kutumika kwenye miaka ya 1,750. Tubitak ni baraza la utafiti wa kisayansi na kiteknolojia la nchini Uturuki.

Michoro ya aina hii inakwenda nyuma hadi kati ya karne ya 4 hadi ya 5.

Msanii wa taaluma mtambuka Celaleddin Celik, ambaye pia ni mbunifu wa makumbusho hiyo pamoja na kituo cha sanaa cha Kazlicesme, alioneshwa kushangazwa kwake na matokeo yaliyopatikana ndani ya mradi huo.

"Hii ilitushangaza sana. Mchakato huu umebadilisha mwenendo mzima wa mradi na kusimamisha kazi zote. Hakuna aliyeweza kuliona hili likitokea," Celik anasema.

“Tunafahamu kuwa Istanbul ina michoro mingi, lakini huu ni wa kwanza kabisa kukutana nao ukiwa ndani ya kuta za mji huu. Imetupa furaha na bashasha sana kwani inaonesha upekee katika historia ya Istanbul,” alisema Omer Arisoy.

‘Furaha ya kukutana na jirani wa kale’

Michoro hiyo inakwenda mbali hadi karne ya 4 na ya 5 wakati jiwe la kaburi na baadhi ya sarafu zinaanzia karne ya 4, 5 hadi ya 11.

Mbali na mabaki ya mifupa katika sarcophagus, mabaki ya binadamu yalipatikana katika kaburi la aina ya cist kutoka kipindi cha Kirumi; hata hivyo, mifupa katika kaburi la matofali ilikuwa imebomoka kabisa.

"Haya ni mabaki ya wenyeji wa kale wa  Zeytinburnu, " Celaleddin Celik anasema.

Kwa mujibu wa chambuzi, moja kati ya mifupa miwili katika makaburi hayo ina umri wa miaka 1,750 , wakati mwingine una miaka 1,775; mwanamke alikuwa na umri wa miaka kati ya 30 hadi 40 na mwanaume alikuwa na miaka kuanzia 40 hadi 50.

“Hawa ni wakazi wa wale wa Zeytinburnu," alisema Celaleddin Celik. Pia meya alionesha furaha ya kukutana na majirani hao wa zamani.

Vipimo vya vinasaba vinafanyika katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Middle East kilichopo Ankara. 

Mabaki ya mifupa ya mwanamume na mwanamke yalipatikana pamoja kwenye vazi la zambarau, lililoonekana kama rangi ya kifalme enzi za utawala wa Byzantine, na kudariziwa kwa rangi ya dhahabu.

Zaidi ya hayo, mwanamume huyo alionesha dalili za mbavu iliyovunjika na aliugua ugonjwa wa baridi yabisi.

Vipimo vya vinasaba vinafanyika katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Middle East kilichopo Ankara.

Jengo hilo linaakisi michoro inayopatikana ndani yake./Picha:Cemal Emden.

"Hadithi ya Usanifu"

Baada ya matokeo hayo ya kusisimua, Arisoy aliamua kubadilisha kituo hicho na kuwa jumba la makumbusho la michoro ili kuonyesha vitu vya kale vilivyopatikana vya kihistoria kwenye tovuti, pamoja na kazi ya pamoja ya Kurugenzi ya Makumbusho ya Akiolojia ya Istanbul na Manispaa ya Zeytinburnu.

"Tulipoanzisha kituo cha sanaa cha Kazlicesme, hatukudhani kuwa tutakuwa na makumbusho ya michoro hapa," Celaleddin Celik anasema.

Likiwa limejengwa mwanzoni mwa miaka ya 1800, jengo hilo la kihistoria lilitumika kama hospitali ya jeshi wakati Ottoman. Baadaye, likabadilishwa na kuwa bwalo, ofisi ya jeshi na sehemu ya biashara kabla halijachukuliwa na manispaa ya Zeytinburnu, mwaka 1984.

Wakati wa Ottoman, jengo hilo lilitumika kama hospitali ya kijeshi./Picha: Cemal Emden.

“Jengo hili la kihistoria linaweka bayana matabaka manne, kila mmoja likiwakilisha vipindi vinne vya kihistoria vya Kirumi, Byzantine, Ottoman na zamu za jamhuri za kisasa,” alisisitiza Meya huyo.

Celik, mbunifu, alisema kuwa ujenzi wa kiambatisho cha jengo la kihistoria ili kuonyesha vitu vipya vilivyogunduliwa nje ya jengo hilo ni mchakato wa kusisimua, unaoendelea, lakini pia ulikuwa na changamoto za usanifu.

"Changamoto za hapa ni za tabaka nyingi. Kwa sababu jengo hilo lilijengwa kama hospitali ya kijeshi wakati wa utawala wa Sultan Abdulhamid II, ambayo ni urithi wa kihistoria. Karibu nayo, mosaic ilipatikana ambayo ina zaidi ya miaka 1,000. ni safu tofauti kabisa. Zote ni mali za kitamaduni na zote zinahitaji kulindwa. Tulibuni nyongeza ya kisasa kwa jengo la kihistoria ambalo linawafikia wote wawili kwa heshima na usikivu wa hali ya juu," Celik alisema.

"Tulipoanza mradi wa Kazlicesme, hatukudhani kungekuwa na makumbusho ya michoro hapa," alisema Celallddin Celik./Picha: Cemal Emden.

"Lazima uwepo bila kuharibu chochote. Kwa upande mwingine, lazima uwepo ndani ya muundo wa kihistoria bila kushindana nayo na bila kupata mbele yake kwa hali ya juu. Pia, unapaswa kuwepo hapa katika lugha ya kisasa bila kuiga muundo wa kihistoria.

Celik pia alibainisha namna muundo wa mbele wa jengo hilo unavyoakisi michoro.

"Mradi huu wa urekebishaji umekuwa hadithi ya usanifu kwetu," alisema.

Kituo cha sanaa cha Kazlicesme kinahusisha maktaba, kituo cha michoro na migahawa.

Sehemu ya chini ya jengo hilo kwa sasa, inatumika kama jumba la sanaa, na makumbusho ya picha iko nje ya jengo hilo.

Ghorofa ya juu ya jumba la makumbusho pia imegeuzwa kuwa maktaba ya sanaa ambayo ina sehemu ya kutazama mandhari ya Istanbul.

Sehemu ya juu ya jengo hilo imetengwa kwa ajili ya kutazama mandhari nzuri ya Istanbul./Picha: Cemal Emden.

Meya alisisitiza kwamba Jumba la Makumbusho la Zeytinburnu litarejesha uhai mpya katika utalii wa kitamaduni wa Istanbul.

"Tunaona kuwa ni jukumu letu kuonesha uwezo wa Zeytinburnu, kuongeza utajiri wake na kukuza maelewano na furaha kati ya watu wetu wa asili zote."

Je, muundo ambao michoro hiyo imegunduliwa ilikuwa ni jumba la kifahari au ngome? Ni kweli kuwa wawili hao waliokuwa wamezikwa pamoja walikuwa ni wapenzi katika kipindi cha Byzantine?

Bado haiwezekani kupata majibu ya maswali haya.

Uchunguzi juu ya uwepo wa michoro, makaburi ya mabaki ya watu ndani yake, bado unaendelea.

TRT Afrika