Bendera ya taifa kupeperushwa nusu mlingoti katika vituo vyote vyenye bendera kote nchini kwa muda wa siku saba kuanzia leo Ijumaa tarehe 7 Februari 2025/ Ikulu:Afrika Kusini 

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameagiza bendera ya taifa kupeperushwa nusu mlingoti katika vituo vyote vilivyo na bendera nchini kote kwa muda wa siku saba kuanzia leo Ijumaa tarehe 7 Februari 2025.

Hi ni kwa ajili ya kuomboleza wanajeshi wa Afrika Kusini waliouwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC baada ya mashambulizi ya waasi wa M23 walioteka Goma mji mkuu wa Kivu Kaskazini.

Wanajeshi hao 14 wa Afrika Kusini walikuwa sehemu ya ujumbe wa kuleta amani mashariki mwa DRC.

Rais Cyril Ramaphosa pia alituma salamu zake za rambirambi kwa wanajeshi wakati akitoa hotuba ya kwanza ya kitaifa, Alhamisi jioni mjini Cape Town.

Wanajeshi hao wa Afrika Kusini walikuwa chini ya Kikosi cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (SAMIDRC).

Kikosi hiko nchini DRC kusaidia serikali ya nchi hiyo kurejesha amani na usalama Mashariki mwa DRC.

Mnamo Mei 2023, SADC iliidhinisha SAMIDRC kuleta utulivu katika eneo hilo, na kuipa mamlaka ya kupambana moja kwa moja na makundi yenye silaha.

Ililenga kuwa na wanajeshi 5,000 kutoka Malawi, Afrika Kusini na Tanzania, lakini ni wanajeshi 1,300 pekee ambao wamepelekwa huko kufikia sasa.

TRT Afrika