Vikosi vya Usalama vya Uturuki vimefanikiwa kuwakamata wanachama wawili wa shirika la kigaidi la FETO.
Katika zoezi lililoratibiwa na Shirika la Kijasusi la Uturuki (MIT) na Kurugenzi Kuu ya Usalama, magaidi waliotambulika kama Mustafa Tan na Mustafa Bircan wamekamatwa.
Tan na Bircan wote wamejihusisha katika tawi la Algeria la shirika la kigaidi.
Operesheni hiyo ya pamoja imesema kwamba, wanachama wa FETO, Tan na Bircan, walihusika katika kupanga na kuratibu shughuli za kundi hilo huko Algeria, wakiwa na uhusiano na viongozi wa shirika nchini Marekani, na kutoa msaada wa kifedha kwa kundi hilo la kigaidi.
Kufanikiwa kwa zoezi hilo, kunaonyesha jitihada endelevu za serikali ya Uturuki katika kusambaratisha mtandao wa kimataifa wa FETO na kuwafikisha wanachama wake katika mkono wa sheria.
Watuhumiwa hao, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Uturuki kwa kujihusisha kwao na vitendo vya shirika la kigaidi.
FETO ni nani?
FETO na kiongozi wake aliye Marekani Fetullah Gulen walipanga mapinduzi yaliyoshindwa mnamo Julai 15, 2016, ambapo watu 251 walipoteza maisha na wengine 2,734 walijeruhiwa.
FETO imekuwa na kampeni ya muda mrefu ya kutaka kupindua serikali kwa kujipenyeza katika taasisi za Kituruki, hasa jeshi, polisi na mahakama.
Marekani imewapa hifadhi idadi kubwa ya wanachama wa FETO, wengi wao ni wale waliokimbia Uturuki baada ya kushindwa kuchukua mamlaka kupitia mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na wanajeshi waliojipenyesha jeshini.
Fetullah Gulen ni mmoja ya mwanachama wa FETO anaetafutwa kwa udi na uvumba na amekuwa nchini Marekani tangu 1999.