Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vikali wito wa Israel wa kuwahamisha wakazi wa kaskazini mwa Gaza kwa lazima na mashambulizi yake yanayoendelea.
Katika taarifa yake, OIC ilisema "Inakataa kabisa na kulaani Israel, wito wa mamlaka inayokalia ya kuwaondoa kwa lazima watu wa Palestina, na majaribio ya kuhamisha mgogoro wa kibinadamu uliozidishwa na uvamizi wa Israel hadi nchi jirani."
Kundi hilo pia "limelaani vikali kuzuiwa kwa matibabu, vifaa vya msaada, na mahitaji ya kimsingi kwa Ukanda wa Gaza kama adhabu ya pamoja, ambayo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa za kibinadamu."
Imesisitiza wito wake kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kukomesha uchokozi wa Israel dhidi ya watu wa Palestina, ambao unaweza kusababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu.
Pia ilisisitiza "umuhimu wa kufungua njia za kibinadamu ili kutoa misaada muhimu kwa Ukanda wa Gaza."
Kuongezeka kwa ukatili dhidi ya Wapalestina
Licha ya onyo la kimataifa, jeshi la Israel siku ya Ijumaa liliamuru wakaazi katika eneo la kaskazini la Gaza lililozingirwa kuhama makazi yao na kuhamia eneo la kusini ifikapo saa kumi jioni kwa saa za huko (1300GMT).
Mzozo kati ya Palestina na Israel ulianza Jumamosi iliyopita wakati Hamas ilipoanzisha Operesheni ya Food AL Aqsa - shambulio la kushtukiza la pande nyingi likiwemo msururu wa kurusha roketi na kujipenyeza Israel kupitia nchi kavu, baharini na angani.
Hamas imesema operesheni hiyo ni ya kulipiza kisasi kuvamiwa kwa Msikiti wa Al Aqsa katika Jerusalem Mashariki inayokaliwa kwa mabavu na kuongezeka kwa ukatili wa walowezi wa Israel dhidi ya Wapalestina.
Jeshi la Israel kisha lilianzisha Operesheni ya Iron Sword dhidi ya malengo ya Hamas ndani ya Ukanda wa Gaza.
Jibu hilo l amashambulio limeenea hadi katika kukata maji na umeme hadi Gaza, na kuzidisha hali ya maisha katika eneo ambalo limekabiliwa na mzingiro tangu 2007, na pia kuamuru zaidi ya Wagaza milioni 1 kuhama kaskazini mwa Gaza katika chini ya masaa 24.