Sanamu ya utambuzi wa mchango wa Baba wa Taifa wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Bara la Afrika, imezinduliwa rasmi kwenye Makao Makuu ya Tume ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa, Ethiopia, Jumapili.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi mbalimbali walishiriki kwenye hafla hiyo ya kihistoria ya uzinduzi wa sanamu hiyo.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi mbalimbali walishiriki kwenye hafla hiyo ya kihistoria ya uzinduzi wa sanamu hiyo.

Marais na viongozi wakuu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika akiwemo Rais wa Zambia Hakainde Hichilema, Rais wa Kenya William Ruto, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU), Moussa Faki, Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete nao walihudhuria uzinduzi huo.

Sanamu hiyo pia inajumuisha kauli mbiu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere inayosema;

"Sisi.....tunataka kuuwasha mwenge na kuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu; ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima palipojaa dharau".

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

"Urithi wa kiongozi huyu wa ajabu unajumuisha kiini cha Pan Africanism, hekima ya kina, na huduma kwa Afrika," Moussa Faki Mahamat Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika alisema.

"Mwalimu lakini pia mpenda amani, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alichukua nafasi kubwa kama mpatanishi katika migogoro ya Afrika, hasa mgogoro wa Burundi," Faki alimaliza.

Aidha, jengo la amani na usalama katika makao makuu ya Umoja wa Afrika sasa limepewa jina la jengo la Mambo ya siasa, Amani na Usalama la Mwalimu Nyerere.

TRT Afrika