Na Coletta Wanjohi
Mkutano wa Kidiplomasia wa Antalya uliwaleta pamoja wakuu wa nchi na serikali, mawaziri, wanadiplomasia, wafanyabiashara, wanazuoni huku majopo na maonesho mbalimbali yaliyoangazia masuala ya siasa, uchumi, elimu na utamaduni yakitamalaki.
Mkutano huo uliofanyika katika mji wa pwani wa Antalya, kando ya bahari ya Mediterenia, ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 140, nyingi zikiwa ni za kiafrika.
Moja ya vivutio vya mkutano huo ni kazi za mikono zilizowakilisha utamaduni wa kiafrika.
Kongamano hilo la Kidiplomasia la Antalya lilitoa fursa ya kubadilishana tamaduni kati ya watu kutoka mataifa mbalimbali duniani, kupitia kazi za sanaa.
Ufinyanzi, ufundi wa chuma, uchongaji, usanifu, sanaa ya nguo ni baadhi ya aina za sanaa za maonyesho katika nchi za Afrika.
Aina za sanaa hii huipa Afrika utambulisho wa kipekee na urithi wa watu wake.
Wageni wengi walipata muda wa kutazama na kufurahia maonesho mbalimbali katika mkutano wa Kidiplomasia wa Antalya.
Mkutano wa mwaka huu ulikuwa na matukio tofauti ikiwemo majopo, maonesho ya sanaa na teknolojia.