Safari nyingi za ndege zimeripoti kubadilisha njia zao za kawaida zilizoratibiwa kwa sababu Sudan haipitikia kwa njia za anga.
"Wakati machafuko yakiendelea, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum ulichukuliwa na waasi, na safari za anga zikapigwa marufuku. Ndege ya Saudi Arabia ilipigwa risasi ilipokuwa ikijiandaa kuondoka nchini,” anaeleza Shakoor Nya Keto, Mwandishi wa Habari wa TV wa Journalingual aliyeko Khartoum.
Nya keto anaeleza kuwa hakuna taarifa rasmi kwani hakuna serikali rasmi lakini anga sasa imezuiwa isipokuwa kwa matumizi ya kijeshi. Safari za ndege za kibiashara kote Sudan zitachukuliwa kuwa tishio.
Ndege ya abiria iliyokuwa ikijiandaa kupaa kutoka Sudan kuelekea Saudi Arabia ilipigwa risasi siku ya Jumamosi. Ndege ya Airbus iliyokuwa ikielekea Saudi Arabia "ilikabiliwa na uharibifu wa risasi... ikiwa na wageni na wafanyakazi ndani ya ndege hiyo" kabla ya safari yake ya kuelekea Riyadh, Saudia Arabia, taarifa ya serikali ya Saudia ilisema.
"Imethibitishwa kuwa watu wote na wafanyakazi kwenye ndege wamefika salama katika Ubalozi wa Saudi nchini Sudan," ilisema taarifa hiyo.
Msaidizi wakati wa Dharura Afrika Mashariki
Ndege ya Emirates ya Airbus A380, inayoweza kubeba abiria 550, ilitua jijini Dar es Salaam, Tanzania, jana usiku kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ikiwa na abiria 514.
"Ndege ilikuwa ikielekea Dubai kutoka Sao Paulo Brazil ikatua kwa dharura Dar es Salaam ili kuongeza mafuta ambayo yataisaidia kukamilisha safari yake kwani anga ya Sudan imefungwa kwa sasa." Wakati akizungumza na TRT Afrika leo mchana, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, TCAA, Hamza Johari alieleza.
"Uwanja wa Ndege ya Tanzania ni mahali pazuri pakutua wakati dharura katika ukanda huu tangu 2017 kwa kuwa ina vifaa na huduma zote za kutegemewa wakati wa dharura kama hiyo, tulikuwa na tukio kama hilo mnamo 2018 wakati ndege ya Mauritius ilishindwa kutua kwa sababu ya hali mbaya ya hewa ikabidi itue JNIA." Johari alieleza zaidi.