Rwanda yapokea dozi 700 za ugonjwa wa Marburg

Rwanda yapokea dozi 700 za ugonjwa wa Marburg

Chanjo hizo zimetolewa na Taasisi ya Sabin.
Dozi 700 za ugonjwa wa Marburg zikiwasili nchini Rwanda./Picha:

Rwanda imepokea chanjo ya ugonjwa wa Marburg, Waziri wa Afya wa nchi hiyo Dkt Sabin Nsanzimana, alisema siku ya Jumapili.

Kulingana na Dkt Nsanzimana, chanjo hizo zitazinduliwa siku ya Jumapili, huku wahudumu wakiwa wa kwanza kupokea chanjo hiyo.

Dkt Nsanzimana ameongeza kuwa chanjo hizo pia zitatolewa kwa watu waliokutana na kugusana na waathirika wa ugonjwa huo hatari.

Chanjo hizo zimetolewa na Taasisi ya Sabin, kulingana na Dkt Nsanzimana.

“Shehena ya kwanza yenye dozi zipatazo 700 zitatumika kwa majaribio kati ya wafanyakazi wa sekta ya afya,” ilisema taasisi hiyo.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Rwanda, asilimia 80 ya maambukizi ya ugonjwa wa Marburg imeripotiwa kati ya wafanyakazi katika sekta ya afya.

TRT Afrika