Ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda ikipakia sehemu ya shehena ya misaada hiyo./Picha: Wengine

Serikali ya Rwanda, kwa kushirikiana na himaya ya Kifalme Hashemite ya Jordan imetoa msaada wa kibinadamu kwa raia wa Gaza.

Msaada huo unahusisha zaidi ya tani 19 za chakula, ikiwemo kile kilichorutubishwa kwa ajili ya watoto, pamoja na madawa mbalimbali.

“Rwanda inaunga mkono jitihada za kumaliza mgogoro wa Gaza na umuhimu wa kuwalinda raia,” ilisema sehemu ya taarifa ya Serikali ya Rwanda.

Hali ya kibinadamu inazidi kuzorota huko Gaza, kufuatia mashambulio ya kila mara kutoka kwa majeshi ya Israeli.

Mbali na vifo, mashambulizi hayo pia yameharibu miondombinu na huduma muhimu zikiwemo za afya .

TRT Afrika