Sehemu ya muonekano wa jiji la Kigali, nchini Rwanda./Picha: Getty

Rwanda inashika nafasi ya kwanza kati ya nchi zilizoweka mazingira wezeshi ya biashara kusini mwa jangwa la Sahara.

Kwa mujibu wa ripoti iitwayo ‘Business Ready’, iliyotolewa na Benki ya Dunia, utafuti unaangazia vigezo mbalimbali, kama vile sera, huduma za kijamii ufanisi.

Ripoti hiyo, iliyotolewa Oktoba 3, 2024, pia inaangazia viashiria vingine kama vile usuluhisho wa migogoro, ushindani wa masoko na biashara ya kimataifa .

Kulingana na utafiti huo wa World Bank, Rwanda iko katika daraja la pili, ikiwa imejikusanyia alama 85.39 kwa kuweka mazingira mazuri ya kufungua biashara nchini humo.

Nchi hiyo ipo katika kundi moja na Hong Kong, New Zealand, Croatia, Romania na Barbados.

Utafiti huo, pia umeiorodhesha Tanzania kati ya nchi zilizofanya vizuri katika kuaanda mazingira mazuri ya ufanyaji wa biashara.

Jiji la Dar es Salaam ambalo ni kitovu cha biashara nchini Tanzania./Picha: Getty

Tanzania iko katika daraja la tatu, kulingana na utafiti wa Benki ya Dunia, ikiwa pamoja na nchi za Costa Rica, Morocco, Lesotho, Mauritius na Samoa.

Nchi hiyo imejikusanyia alama 87.19, kwa kuwa na sera nzuri za ufunguaji na ufanyaji wa biashara.

Utafiti huo, umeangazia hali ya ufanyaji wa biashara katika nchi 50 duniani.

TRT Afrika na mashirika ya habari