Nchi hizo mbili zimekuwa zikitupiana lawama kuhusu machafuko katika eneo la Mashariki mwa DRC./Picha: AP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe amedai kuwa waziri mwenzake kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amegoma kutia sahihi mkataba unaolenga kumaliza machafuko katika eneo la Mashariki ya DRC.

Kikundi cha M23, kinachoongozwa na Watutsi kimeongoza machafuko hayo toka mwaka 2022.

Hata hivyo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Umoja wa Mataifa, wamekuwa wakiituhumu Rwanda kwa kukiunga mkono kikundi hicho.

Kwa upande wake, Rwanda ambayo imekana tuhuma za kukiunga mkono kikundi cha M23, inasema kuwa imechukua hatua za kujihami, huku ikiituhumu DRC kwa kwa kushirikiana na na kikundi cha Kihutu cha FDLR.

'Tuko tayari kuweka sahihi'

Nchi zote zilishiriki katika mchakato wa maridhiano uliofanyika mwishoni mwa mwezi wa Agosti, ukiwa unalenga kupunguza machafuko hayo.

Nduhungirehe ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa wajumbe wa mazungumzo hayo akiwemo mkuu wa idara ya upelelezi ya kijeshi wa Kongo wamekubaliana na kutia saini mpango wa "kuiondoa FDLR."

Kulingana na Waziri huyo, mkataba huo ulipaswa kutiwa saini na mawaziri mnamo Septemba 14.

"Tuko tayari kutia sahihi...lakini Waziri wa Congo amekataa kufanya hivyo. Mwanzoni alitoa maoni yake kuhusu ripoti yake, lakini baadaye akasema hakubaliani nayo."

TRT Afrika