Rwanda yaanza maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari ya 1994, mauaji ya halaiki yaliyoratibiwa na Wahutu wenye itikadi kali dhidi ya Watutsi walio wachache kwa muda wa siku 100 za umwagaji damu.
Zaidi ya watu 800,000 waliuawa katika mashambulizi ya mauaji ambayo yalishuhudia familia na marafiki wakigeukana katika moja ya matukio ya giza kabisa mwishoni mwa karne ya 20.
Miongo mitatu baadaye, taifa limejenga upya chini ya utawala wa Rais Paul Kagame, lakini historia ya kutisha ya mauaji ya halaiki inaendelea, ikirejea katika eneo lote.
Kwa mujibu wa mila, Aprili 7 - siku ambayo Wahutu wenye msimamo mkali na wanamgambo walianzisha mauaji ya kutisha mwaka 1994 - itaadhimishwa na Kagame kuwasha mwenge wa ukumbusho kwenye Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari ya Kigali, ambapo zaidi ya waathiriwa 250,000 wanaaminika kuzikwa.
Kagame ambaye jeshi lake la waasi la Rwandan Patriotic Front (RPF) lilisaidia kukomesha mauaji hayo, atatoa hotuba na kuweka mashada ya maua kwenye makaburi ya halaiki, huku baadhi ya viongozi wa kigeni wakihudhuria kile kilichopewa jina la "Kwibuka (Kumbukumbu) 30".
Matukio ya Jumapili yaliashiria mwanzo wa wiki ya maombolezo ya kitaifa, huku Rwanda ikisimama vyema na bendera za taifa zikipeperushwa nusu mlingoti.
Katika siku hizo, muziki hautaruhusiwa katika maeneo ya umma au kwenye redio, huku matukio ya michezo na filamu zimepigwa marufuku kutoka katika matangazo ya TV, isipokuwa kama zimeunganishwa kwenye ukumbusho.
Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, miongoni mwa wengine, pia watafanya sherehe za ukumbusho.