Mwezi Julai, Rwanda ilithibitisha kwa mara ya kwanza uwepo wa maambukizi mapya ya Mpox ndani ya mipaka yake/ Picha: Wizara ya afya Rwanda    

Rwanda imeanza kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya Mpox, ikiwalenga zaidi watu walio katika mazingira hatarishi.

" Kama sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na maambukizi ya Mpox, Wizara ya Afya imezindua kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo kwa watoa huduma wa afya, wafanyabiashara wa mipakani, wafanyakazi katika sekta ya utalii na wageni na vikundi vingine vilivyo hatarini," Wizara hiyo imesema katika akaunti yake ya X.

Mwezi Julai 2024, Rwanda ilithibitisha kwa mara ya kwanza kesi mpya za Mpox ndani ya mipaka yake. Hata hivyo, hakuna vifo vilivyoripotiwa .

Wizara ya afya nchini Rwanda imesisitiza kuwa mtu yoyote yule anaweza kuambukizwa Mpox ikiwa vimelea vya ugonjwa huo hupitia kwa njia za kugusana na njia za maji.

Ugonjwa huo uliibuka tena ulimwenguni mnamo 2022, kulingana na Kituo cha Matibabu cha Rwanda. Tangu 2023, Mpox imeenea katika nchi tofauti zinazopakana na Rwanda.

Mnamo tarehe 14 Agosti 2024, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), alitangaza kuibuka tena kwa Mpox kuwa dharura ya kiaafya yenye kuhitaji mwitikio wa kimataifa.

Chanjo za Mpox zimeanza kusamabazwa katika tofauti barani Afrika, huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiongoza kwa idadi ya maambukizi.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

TRT Afrika